Mwili wa kiongozi wa zamani wa upinzani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Etienne Tshisekedi umewasili mji mkuu wa Kishasa.
Mwili huo ambao umetokea nchini Ubelgiji ikiwa ni miaka miwili tokea kufariki kwake.

Tshisekedi aliyefariki akiwa na umri wa miaka 84, alikuwa kiongozi wa upinzani kwa miongo kadhaa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kabla ya kifo chake mwaka 2017, nchini Ubelgiji.
Wafuasi wake wanasema alikuwa tishio kubwa kwa Rais wa zamani Joseph Kabila hata maiti yake ilibidi kubaki nje ya nchi.

Kurudi kwa mwili wake kunatimiza mojawapo ya ahadi za mwanawe Felix Tshisekedi, ambaye bila kutarajia aliingia madarakani kama Rais wa Congo mapema mwaka huu.
Maelfu ya watu wanatarajiwa leo kuhudhuria ibada ya kuuaga mwili wa Tshisekedi katika uwanja wa mpira mjini Kinshasa amako viongozi wa mataifa sita ya kiafrika wanatarajiwa kuhudhuria mazishi hayo yatakayofanyika rasmi kesho Jumamosi.
Kinshansa, Congo.