We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Showing posts with label SIASA. Show all posts
Showing posts with label SIASA. Show all posts

Monday, October 14, 2019

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi.

Leo tumekuletea habari njema ni kuwa tayari App mpya ipo playstore na unaweza kuidownload hapa chini ili kuendelea kupata habari zetu.

BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD APP YETU MPYA UKISHA BOFYA BONYEZA NENO OPEN IN PLAYSTORE KISHA INSTALL APP YETU MPYA!! NI RAHISI TU

Wednesday, October 2, 2019

Mbunge CCM awajibu wanaosema hali ni ngumu

Mbunge wa Jimbo la Kinondoni,Abdallah Mtolea, amewatia moyo wale wote wanaolalamika kuhusu hali ngumu, kwakuwa ugumu wa maisha ndiyo kipimo cha maendeleo kwa mtu na kwamba hakuna nchi yoyote ambayo ilishawahi kuendelea bila kupitia nyakati ngumu

Mbunge Mtolea ametoa kauli hiyo, wakati akizungumza kwenye kipindi cha East Africa BreakFast cha East Africa Radio, ambapo amekiri kuwa hali ni ngumu na kuwataka wananchi wawe wavumilivu.
"Wengi wanasema hali ni ngumu ila niwaambie, hakuna nchi ambayo iliendelea kwenye hali ambayo ni nyepesi, lazima tupate maendeleo kwenye hali ngumu." amesema Mtolea.
Aidha akizungumzia suala la kuhama chama, Mtolea amesema kuwa hana mpango huo na ataendelea kuwa ndani ya Chama Cha Mapinduzi.
''2020 nitaendelea kuwa Chama Cha Mapinduzi, uzuri ukiwa CCM ukienda kwa kiongozi wa Serikali unakuwa kama umeenda kwa Baba, yaani ndiyo maana kila kitu kinaenda kiurahisi'' amesema Mtolea.

MAKONDA KUBANANISHWA MBELE YA DR. BASHIRU, MAMA SAMIA "ATUELEZE AMEFANYA NINI? "

Bonyeza play hapa chini kutazama zaidi pia tembelea app hii kila Mara kusoma Habari Mpya

ACT-Wazalendo wajipanga kupinga uteuzi wa mkurugenzi NEC mahakamani - VIDEO



Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe amesema chama hicho kimemuagiza wakili, Jebra Kambole kuangalia misingi ya kisheria ili kufungua kesi ya kupinga uteuzi wa mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Dk Wilson Charles.

Ametoa kauli hiyo leo Jumatano Septemba 2, 2019 muda mfupi baada ya kutoka kusikiliza kesi ya kupinga ukomo wa urais iliyofunguliwa na Dezydelius Mgoya ambayo chama hicho kimeomba kujumuishwa.
Akiwa katika viwanja vya Mahakama Kuu, Dar es Salaam Zitto amesema wameshangazwa na uamuzi wa Rais John Magufuli kumteua Charles aliyewahi kugombea ujumbe wa halmashauri kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (NEC).
“Suala hili la wasimamizi wa uchaguzi ambao ni wanachama wa vyama vya siasa kuteuliwa lipo mahakamani, kuna kesi imefunguliwa na Bob Wangwe na wanasheria pamoja na wanaharakati.”
“Mahakama ikatoa amri kwamba  wasimamizi wa uchaguzi hawapaswi kuwa wanachama, makada au mashabiki  wa vyama vya siasa,” amesema Zitto.


Amesema kitendo cha kuteuliwa kwa Wilson ni dharau kwa mahakama ambayo imeshatoa uamuzi kuwa hawapaswi kusimamia uchaguzi.
Amebainisha kuwa kulingana na suala hilo kuwa muhimu, wanashauriana na vyama vingine vya siasa kwa ajili ya kuchukua hatua za kisheria kuzuia uteuzi huo.
“Tumeshamuagiza Kambole atazame misingi ya kisheria ili kuhakikisha tunazuia uteuzi. Tunahitaji uchaguzi huru tunaangalia namna bora ya kuweza kuchukua hatua za kisheria.”
“Tunataka wakili atazame jambo hili kulingana na uamuzi wa mahakama katika kesi ya awali (ambayo Serikali ilikata rufaa) na sasa tunasubiri uamuzi wa rufani ili kuhakikisha tunazuia uteuzi wa wanasiasa kusimamia uchaguzi,” amesema Zitto.

Wazee CHADEMA Wavunja Ukimya

Baraza la Wazee la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), limeitaka serikali kurejea ahadi yake ya kumalizia mchakato wa katiba mpya iliyoitoa mwaka 2015 wakati wa uchaguzi mkuu.
Wazee hao wamedai kuwa  mchakato huo bado una umuhimu mkubwa kwa Watanzania.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Baraza hilo, Hashim Juma Issa, alidai kushangazwa na ukimya wa serikali kuhusu mchakato huo ambao uligharimu fedha nyingi za Watanzania.

Wazee hao wanadai kusitishwa kwa mchakato huo ni hasara kubwa kwa Taifa kwa kuwa mchakato huo ulishaanza na umegharimu fedha nyingi, hivyo kutaka uendelezwe kwa maslahi ya Taifa.

Katika hatua nyingine, wazee hao wamelalamikia kuingiliwa kwa mikutano ya wabunge wa chama hicho na Jeshi la Polisi, wakidai kitendo hiko ni ukiukwaji wa misingi ya demokrasia nchini na kounya kuwa vitendo hivyo vinaweza kupelekea uvunjifu wa amani.

Kuhusu uchaguzi wa serikali za mitaa,  wameapa kulinda kura kwa madai ya kuchoka kuibiwa kura kila uchaguzi unapofika, na kulionya Jeshi la Polisi kuwa waangalifu katika uchaguzi huo ili kuepusha uvunjifu wa amani.

Profesa Tibaijuka kurejesha shilingi 1.6 bilioni za mgao wa Rugemarila

Mbunge wa Muleba Kusini (CCM), Profesa Anna Tibaijuka amesema uongozi wa Shule ya Sekondari Barbro Johansson Model Girls utarejesha fedha za msaada walizopokea  kutoka kwa mfanyabiashara, James Rugemarila ili aweze kutoka gerezani.

Profesa Tibaijuka amesema hayo kupitia Kituo cha televisheni cha Azam TV.

Amesema uongozi wa shule hiyo umekaa kikao na kuamua kurejesha  fedha hizo walizopokea ili kumsaidia  mtuhumiwa huyo anayekabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi kutoka gerezani.

Alipoulizwa kama fedha walizopewa msaada zilikuwa hazijatumika hadi sasa,  Profesa Tibaijuka amesema licha ya fedha hizo kutumika kulipa deni la kujenga bweni la shule lakini zitatafutwa na zitarejeshwa.

==>>Msikilize hapo chini

Tuesday, October 1, 2019

Kauli ya CHADEMA kuhusu Mkurugenzi mpya NEC

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimetoa maoni yake juu ya Mkurugenzi mpya wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Dkt Wilson Charles, na kwamba kwa sasa wamejipanga kushughulika naye kuelekea katika Uchaguzi Mkuu ujao.

Akizungumza na EATV&EA Radio Digital  leo Oktoba 1, 2019, Mkurugenzi wa Mawasiliano, Itifaki na Mambo ya Nje wa chama hicho John Mrema, amesema kwa sasa hawezi kumzungumzia Mkurugenzi aliyepita na badala yake wanamtakia heri na fanaka kwa majukumu yake mengine.
"Aliyepita ameshapita, kwa hiyo hata tukimzungumzia haisaidii, tumtakie kila la heri huko anakoenda kupangiwa kazi nyingine, tushughulike tu na huyu ambaye yupo na tutakayekuwa naye kwenye uchaguzi muda mchache ujao" amesema Mrema.
Mara kwa mara chama hicho kilikuwa kikiingia kwenye migogoro na aliyekuwa Mkurugenzi wa NEC Dkt Athuman Kihamia.

TUMEBORESHA APP YETU, TAFADHALI BOFYA HAPA CHINI KUDOWNLOAD APP YETU MPYA ILI KUENDELEA KUPOKEA HABARI KWA WAKATI NA KUTAZAMA MECHI ZOTE LIVE ( UKISHA BOFYA, BONYEZA NENO OPEN IN PLAY STORE KISHA INSTALL )

BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YETU MPYA BURE KABISA

RC Gambo azungumzia kugombea ubunge Arusha Mjini


Mkuu wa mkoa wa Arusha (RC) nchini Tanzania, Mrisho Gambo ameweka hadharani hana nia ya kugombea ubunge wa Arusha kama ambavyo uvumi umekuwa ukisambaa.

Akizungumza katika mkutano wa Jumuiya ya wanawake wa CCM (UWT)  mko Arusha jana usiku Jumatatu Septemba 30,2019, Gambo alisema nafasi ya Mkuu wa mkoa wa Arusha ambayo ameteuliwa na Rais John Magufuli inamtosha.
"Nafasi niliyonayo ni kubwa, wakuu wa wilaya wote wapo chini yangu, wabunge wote wapo chini na taasisi zote za Arusha zipo chini yangu, wabunge wamekuwa wakija kuniomba niwasaidie lakini mimi kama RC naagiza tu," alisema.
Gambo alisema bado anahitaji kuunyoosha mkoa wa Arusha.
Naye Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Arusha, Joseph Masawe alisema tangu Mkuu huyo wa mkoa afike Arusha, mji wa Arusha umetulia hakuna vurugu na watendaji wa serikali wanafanya kazi nzuri kutekeleza ilani.
Kwa muda mrefu, Gambo ambaye amekuwa na makazi ya kudumu eneo la kwa Mrombo katika jiji la Arusha amekuwa akitajwa kugombea ubunge wa Arusha hasa kutokana na jitihada zake kuboresha huduma za kijamii katika jiji la Arusha.
Tayari Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema alikwisha kumkaribisha Gambo kwenye kinyang'anyiro cha ubunge katika uchaguzi mkuu ujao 2020 huku akimweleza ajipange vizuri.
Lakini pia Kamanda wa vijana wa CCM mkoa Arusha, Phelemon Mollel ambaye pia amekuwa akitajwa kutaka kuwania tena jimbo hilo mara kadhaa amekuwa akimtaja Gambo huenda atagombea naye ndani ya CCM.
TUMEBORESHA APP YETU, TAFADHALI BOFYA HAPA CHINI KUDOWNLOAD APP YETU MPYA ILI KUENDELEA KUPOKEA HABARI KWA WAKATI NA KUTAZAMA MECHI ZOTE LIVE ( UKISHA BOFYA, BONYEZA NENO OPEN IN PLAY STORE KISHA INSTALL )

BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YETU MPYA BURE KABISA

Monday, September 30, 2019

TAARIFA MPYA TAFADHALI TUNAKUOMBA UISOME MUDA HUU


Ndugu msomaji na mtembeleaji wa app yetu, tunaomba radhi kwa wale mlio kuwa hampati Habari kwa wakati ni kutokana na maboresho tuliyokuwa tukifanya hivyo kwasasa tuna kushauri kudownload app yetu MPYA hapa chini ili kuendelea kupata Habari kwa wakati.

TUMEBORESHA APP YETU, TAFADHALI BOFYA HAPA KUDOWNLOAD APP YETU MPYA ILI KUENDELEA KUPOKEA HABARI KWA WAKATI NA KUTAZAMA MECHI ZOTE LIVE ( UKISHA BOFYA, BONYEZA NENO OPEN IN PLAY STORE KISHA 
INSTALL )


AU HAPA CHINI

Sunday, September 29, 2019

Mbunge CCM amuita Fatma Karume ili amshauri

Mbunge wa CCM kutoka jimbo la Temeke, Abdallah Mtolea, amesema kwa sasa hawezi kumshauri chochote, aliyekuwa Wakili wa kujitegemea Fatma Karume juu ya chama gani cha siasa ambacho anaweza kujiunga nacho kwa sasa endapo atatangaza kujiingia kwenye siasa.

Mbunge Mtolea ametoa kauli hiyo wakati akizungumza kwenye kipindi cha Kikaangoni kinachoruka kupitia kwenye kurasa za Facebook na Youtube ya EATV, ambapo amesema anaweza kumshauri Fatma Karume chama cha kwenda endapo atamfuata na kujua malengo yake.
"Kuhusu Fatma Karume kusimamishwa Uwakili Tanzania Bara, kwenye sheria tunafundishwa kukubaliana na hukumu yeyote inayotolewa, ila kama hujakubaliana nayo huwezi kusema hadharani kwamba hukubaliani nayo, kuhusu kumshauri kwa sasa ajiunge chama gani siwezi kumshauri kwanza sijui anataka kwenda kufanya nini kwenye siasa" amesema Mtolea
"Kama akija kwangu nitamsikiliza anataka kufanya nini na anataka kwenda kugombea au lah unajua si kila mwanasiasa anataka kuingia kwenye siasa anataka kuwa kiongozi, lazima nijue anataka kwenda wapi kama anataka kuwa mkosoaji wa Serikali, nitamueleza chama cha kwenda" amesema Mbunge Mtolea

Saturday, September 28, 2019

CHADEMA watuma ombi kwa Kangi Lugola

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimemuomba Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Kangi Lugola, kufuatilia rufaa za malalamiko walizowahi kuziwasilisha ofisini kwake juu ya zuio la Jeshi la Polisi la kufanya mikutano ya hadhara na  kisiasa.

Kauli hiyo imetolewa leo Septemba 28, 2019 na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa chama hicho, Tumaini Makene wakati akizungumza na EATV &EA Radio Digital, ambapo amesema kuwa wameshangazwa na kauli ya Waziri Lugola aliyoitoa hivi karibuni ya kwamba hajawahi kupokea barua kutoka vyama vya upinzania, kuhusu kuzuiliwa kufanya mikutano yao.
''Kama kweli anataka kutenda haki, afanyie kwanza kazi na maamuzi ya rufaa ambazo ziko mezani kwake kama akibisha, sisi tuko tayari kumpelekea  vielelezo vya namna ambavyo madiwani na wabunge wetu ambao wameshapeleka malalamiko ofisini kwake baada ya kuwa wamezuiliwa kufanya mikutano'', amesema Makene.
Waziri Lugola alitoa kauli hiyo Septemba 26 Jijini Dodoma baada ya kuzindua ofisi ya Kituo cha Sheriaa na Haki za Binadamu (LHRC), ambapo alisema kuwa, ''tangu nimeteuliwa sijawahi kupokea hata rufaa kulalamika kuwa wamenyimwa haki, badala yake wanakurupuka na kulalamika sasa mimi nifanyeje'', alisema Lugola.

Waziri Lugola: Sijawahi kupokea rufaa ya kulalamika kunyimwa kufanya mikutano, Wanakurupuka

Waziri wa Mambo ya Ndani nchini Tanzania,  Kangi Lugola amesema wanaolalamika na kuanza kufanya maandamano na mikutano wanavyotaka wao bila kibali ni  lazima wakutane na mkono wa sheria kwani polisi iko imara na hawawezi kuachwa.

amesema Lugola alisema sheria zikifuatwa hakuna  shida itakayotokea lakini kinyume na hapo mambo yanakuwa tofauti.

Kiongozi huyo ametoa kauli hiyo juzi baada ya kuzindua ofisi ya Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) mjini Dodoma.

Alisema sheria inawataka watu wanaotaka kukusanyika kulipa taarifa Jeshi la Polisi, wakiona kimya wanaendelea ila wakipewa barua ya zuio wanatakiwa kusitisha shughuli hizo na kukata rufaa kwa waziri mwenye dhamana ya wizara hiyo.

amesema hajawahi kupokea barua yoyote kutoka chama cha siasa kulalamika kuzuiwa kufanya mikutano ya hadhara au maandamano.

“Tangu nimeteuliwa sijawahi kupokea hata rufaa kulalamika kuwa wamenyimwa haki badala yake wanakurupuka na kulalamika sasa mimi nifanyeje,” amesema Lugola

“Tunao polisi imara, hakuna polisi anayeweza kuwakimbia watu hata kidogo lazima wasonge mbele, sasa hapo ndio mtasikia huyu kaumia au kaumizwa yote ni kwa sababu hawafuati sheria,” alisema Lugola.

Friday, September 27, 2019

Vyama vya siasa vyapewa mwongozo

Asasi za Kiraia nchini Tanzania imevitaka vyama vya siasa nchini kuhakikisha wanazingatia ilani mpya iliyozinduliwa na kuitumia katika uchaguzi wa Serikali za mitaa na uchaguzi mkuu wa 2020 na chama chochote kitakachokaidi mwongozo huo kitakuwa kimejitoa chenyewe.

Akizungumza leo Septemba 27, 2019 wakati wa uzinduzi wa ilani hiyo, Mwakilishi wa Asasi za Kiraia, Deus Kibamba, amesema lengo la AZAKI ya uchaguzi  ni kuhakikisha watanzania wanabainisha vipaumbele vikuu vya kuchagua viongozi watakaotekeleza vipaumbele hivyo na kwamba waitumie ili kulinda maslahi mapana ya wananchi.
''Mambo tuliyoyaweka kwenye ilani tumewahi ili kusudi ilani zinazotengenezwa na vyama zibebe haya mambo, chama ambacho hakiweki haya mambo kwenye ilani zao kitakuwa kimekalia kuti kavu kwa upande wetu kwahiyo sisi tunachagua chama ambacho ilani zao zitakuwa zimesheheni mambo ambayo tumeyapendekeza'', amesema Kibamba.
Kibamba amesema kuwa ilani hizo walizoziandaa zimebeba ajenda zao kabla na hata baada ya uchaguzi kwani inatoa mwongozo kwa Serikali na vyama siasa pamoja na wagombea  watakaoshinda katika chaguzi zijazo kutekeleza na matakwa ya kijamii na kuleta manufaa kwa maendeleo ya taifa.

Lema amuunga mkono IGP Sirro

Mbunge wa Arusha Mjini, Gobless Lema amesema kuwa huenda IGP Simon Sirro ameona anapaswa kusimamia ukweli juu ya baadhi ya Makamanda wake kukiuka misingi na kujihusisha na vitendo vya siasa nchini.

Lema amesema hayo kufuatia kauli ya tahadhari ya IGP Sirro kwa Makamanda wa Polisi nchini wanaojihusisha na masuala ya siasa, lakini akihoji suala la vikao vya kinidhamu vya jeshi la Polisi na Makamanda wake wa nchi nzima kufanyika hadharani badala ya ndani.
"Naona IGP Sirro atakuwa ameona utendaji wake utakuwa mbaya akiachilia hili, kwa sababu bila Polisi imara taifa litaangamia au pengine amejua siku zake za kuwa kazini zinahesabika", amesema Lema alipozungumza na EATV & EA Radio Digital.
Ameendelea kusema kuwa hata baadhi ya makamanda katika mikoa hawaweki wazi na kuonyesha vitendo vya siasa lakini ndani yake kuna siasa wanazifanya kwa ndani.
Septemba 24 katika ufunguzi wa kikao cha Makamishina wa Polisi  na Makamanda wa Mikoa, IGP Sirro alisema kuwa kulingana na amri za jeshi hilo, askari atakayejihusisha na siasa lazima wenzake watamshangaa, "changamoto ni baadhi yetu kujihusisha na siasa, katiba hairuhusu na kanuni za Polisi zipo wazi, polisi sio wanasiasa tujikite kwenye majukumu yetu".
"Watu wanataka kusikia unasema nini, wewe sio mwanasiasa unajiaibisha mwenyewe na unafanya hivyo kwasababu upo kwenye nafasi hiyo, tukikutoa hapo hutaweza kufanya, kuna watu wanatafuta umaarufu wa kisiasa tu", alisema Sirro.

Siri ya ukimya wa Joshua Nassari

Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Kanda ya Kaskazini, kimeeleza chama hicho bado kinashirikiana na aliyekuwa Mbunge wake wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari, na kueleza wala hakijamtenga kwa kuwa alivuliwa Ubunge.

Kauli hiyo ya CHADEMA imetolewa na Katibu wa CHADEMA Mkoa wa Arusha Elisa Mungure, wakati akizungumza na EATV na EA Radio Digital ambayo ilitaka kujua siri ya ukimya ya Joshua Nassari, na tangu alipovuliwa Ubunge na Spika Job Ndugai.
Katibu wa CHADEMA Arusha Elisa Mungure amesema "siri ya ukimya wa Nassari ni kwamba unapokuwa Mbunge unapata nafasi ya kuzungumza na vyombo vya habari na kufanya shughuli za maendeleo kwenye jamii, na anaonekana akipiga kelele hiyo fursa hana baada ya kunyanganywa Ubunge wake,  amekuwa mwanachama wa kawaida ndani ya CHADEMA, ndiyo maana amekuwa kimya"
"Kuhusu kumtenga hizo taarifa ni za kupikwa unawezaje kumtenga mwanchama kama Nassari, na kama kuna mambo ambayo tunahitaji uzoefu wake huwa tunamuita na anatupa ushauri wake" ameongeza Katibu wa CHADEMA Mkoa wa Arusha Elisa Mungure
Marchi 2019 Spika Ndugai alitangaza kumvua Ubunge Joshua Nassari kwa kushindwa vikao vitatu vya mahudhurio ndani ya Bunge.

Sunday, September 22, 2019

Friday, September 20, 2019

Mkuu wa wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya Aamuru Viongozi Wanne wa CHADEMA Wakamatwe

Mkuu wa wilaya ya Hai, Mhe. Lengai Ole Sabaya ameagiza viongozi wanne wa CHADEMA mkoani Kilimanjaro akiwemo Mbunge wa Viti Maalum, Mhe. Lucy Owenya kukamatwa baada ya kutembelea shule ya Sekondari Rundugai wilayani humo kwa madai ya kufanya siasa kinyume cha utaratibu.

Wengine waliokamatwa ni mwenyekiti wa Halmashauri ya Hai, Helga Mchomvu, Katibu wa Mbunge wa Hai, Irene Lema na Diwani wa Machame kaskazini, Clement Kwayu.

Sabaya amesema kuwa viongozi hao walikwenda katika shule hiyo leo Ijumaa asubuhi kwa madai ya kuzungumza na wanafunzi na kutoa misaada, bila mkurugenzi wa Halmashauri hiyo kuwa na taarifa.


Amesema, kwa mujibu wa maelekezo yaliyotolewa na Serikali,yeyote anayetaka kutoa misaada katika shule yeyote atoe taarifa kwa mkurugenzi wa Halmashauri ili misaada hiyo ijulikane lengo lake na iweze kuratibiwa

Monday, September 16, 2019

Kauli ya kwanza ya JPM, Lissu kukosa Ubunge ( VIDEO )

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametoa kauli ya kwanza, tangu kuchaguliwa kwa Mbunge wa Singida Mashariki Miraji Mtaturu ambaye amechukua nafasi ya Tundu Lissu.


Rais Magufuli ametoa kauli hiyo jijini Dar es salaam wakati wa uzinduzi rada mbili za kuongozea ndege, ambapo amesema jimbo hilo lilikuwa halina mwakilishi.
Rais Magufuli amesema kuwa "nimefurahi kumuona Mbunge wa CUF, lakini nimefurahi kumuona Mbunge ambaye jimbo lilitelekezwa lililokuwa la Tundu Lissu (Miraji Mtaturu), ameingia na kazi, saa nyingine majimbo yanakosa uwakilishi."
"Siku ile ulitoa maagizo Spika tushughulikie tatizo la maji kule, nakuahidi tutashughulikia maji katika jimbo lile (Singida Mashariki) ili yale yaliyochelewa yakamilike kwa haraka haraka." ameongeza Rais Magufuli
Hivi karibuni Bungeni jijini Dodoma, Spika wa Bunge la Tanzania Job Ndugai alimuapisha Miraji Mtaturu kuwa Mbunge wa Singida Mashariki

Sunday, September 15, 2019

"CCM WANATUMIA MBINU YA 442, TUWE NGANGARI KINOMA"- LIPUMBA

Bonyeza play hapa chini kutazama zaidi pia tembelea app hii kila Mara kusoma habari mpya

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list