Asasi za Kiraia nchini Tanzania imevitaka vyama vya siasa nchini kuhakikisha wanazingatia ilani mpya iliyozinduliwa na kuitumia katika uchaguzi wa Serikali za mitaa na uchaguzi mkuu wa 2020 na chama chochote kitakachokaidi mwongozo huo kitakuwa kimejitoa chenyewe.
Akizungumza leo Septemba 27, 2019 wakati wa uzinduzi wa ilani hiyo, Mwakilishi wa Asasi za Kiraia, Deus Kibamba, amesema lengo la AZAKI ya uchaguzi ni kuhakikisha watanzania wanabainisha vipaumbele vikuu vya kuchagua viongozi watakaotekeleza vipaumbele hivyo na kwamba waitumie ili kulinda maslahi mapana ya wananchi.
''Mambo tuliyoyaweka kwenye ilani tumewahi ili kusudi ilani zinazotengenezwa na vyama zibebe haya mambo, chama ambacho hakiweki haya mambo kwenye ilani zao kitakuwa kimekalia kuti kavu kwa upande wetu kwahiyo sisi tunachagua chama ambacho ilani zao zitakuwa zimesheheni mambo ambayo tumeyapendekeza'', amesema Kibamba.
Kibamba amesema kuwa ilani hizo walizoziandaa zimebeba ajenda zao kabla na hata baada ya uchaguzi kwani inatoa mwongozo kwa Serikali na vyama siasa pamoja na wagombea watakaoshinda katika chaguzi zijazo kutekeleza na matakwa ya kijamii na kuleta manufaa kwa maendeleo ya taifa.
No comments:
Post a Comment