We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Showing posts with label TOP STORY. Show all posts
Showing posts with label TOP STORY. Show all posts

Wednesday, July 17, 2019

Mrema aeleza hitaji lake kwa Rais Magufuli

Baada ya kumaliza muda wake wa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Parole, Augustino Mrema, amesema yupo tayari kuendelea, endapo Rais Magufuli atamteua tena.

Mrema ameyasema hayo leo Julai 17, 2019 kupitia kipindi cha East Africa Drive cha East Africa Radio, ambapo ameeleza mpango wake wa kuwatoa wafunga takribani 5000.

''Pamoja na kipindi changu kuisha lakini nipo tayari kuendelea endapo Rais Magufuli ataniteua tena na lengo ni kutimiza ndoto yangu ya kutoa wafungwa zaidi ya 5000'', amesema.
Aidha Mwanasiasa huyo nguli ameongeza kuwa Katika kipindi chake cha miaka mitatu kilichomalizika Julai 16, 2019, amefanikiwa kuwatoa wafungwa zaidi ya 600.
Kwa upande mwingine Mrema ameiomba Wizara ya Mambo ya Ndani kupitia kwa Mawaziri wake ambao ni Mh. Kangi Lugola na Naibu wake Hamad Masauni, iharakishe michakato ya kuwatoa wafungwa wanaopendekezwa na Bodi ya Parole ili kupunguza msongamano wa wafungwa kwenye Magereza nchini.
Mrema aliyeteuliwa na Rais John Magufuli, kuongoza bodi hiyo Julai 16, 2016, hivyo jana Julai 16, 2019, alitimiza kipindi cha miaka  mitatu cha kuongoza bodi hiyo.

Tuesday, July 16, 2019

IGP afanya ziara Tabora, sikiliza alichosema kuhusu mikutano ya ndani

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro amefanya ziara ya kikazi mjini Tabora, pamoja na mambo mengine amezungumzia suala la mikutano ya ndani ya siasa na kusema kuwa mikutano hiyo haujakatazwa.

Bonyeza play hapa chini kutazama zaidi pia tembelea app hii kila Mara kusoma habari mpya.

Rais Magufuli awapa siku tano Mawaziri wawili

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ametoa siku 5 kuanzia leo July 16, 2019 kwa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano na Wizara ya Fedha na Mipango kuhakikisha vifaa vya ujenzi wa chelezo ya kujengea meli na vifaa vya ukarabati wa meli vilivyokwama katika Bandari ya Dar es Salaam kutokana na mchakato wa kikodi vinafikishwa katika Bandari ya Mwanza.
Rais Magufuli ametoa agizo hilo alipotembelea Bandari ya Mwanza kwa lengo la kukagua maendeleo ya ujenzi wa chelezo, ukarabati wa meli 5 na ujenzi wa meli mpya katika Ziwa Victoria yanayofanywa na kampuni 2 za ukarasi kutoka Jamhuri ya Korea kwa gharama ya shilingi Bilioni 152 kwa ajili hiyo.
Akiwa bandarini hapo, Rais Magufuli ameeleza kutofurahishwa na ucheleweshaji wa takribani mwezi mmoja wa makontena 58 yenye vifaa vya ujenzi vilivyoagizwa na kampuni za ukandarasi za Korea Total Marine Innovation (KTMI) na STX JV SAEKYUNG Construction Ltd za Korea kwa sababu ya kusubiri msamaha wa kodi na amemtaka mkandarasi huyo aache visingizio.
Meneja wa mradi wa ujenzi wa chelezo na ukarabati wa meli Mhandisi Abel Gwanafyo amesema ujenzi wa chelezo pamoja na ukarabati wa meli ya MV Victoria na Mv Butiama umepangwa kukamilika ifikapo Machi 2020.
Kuhusu ujenzi wa meli mpya Meneja Mradi wa ujenzi wa Meli hiyo Mhandisi Vitus Mapunda amesema maandalizi ya vifaa vya meli hiyo itakayokuwa na uwezo wa kubeba tani 400 za mzigo, abiria 1,200 na magari makubwa na madogo 23 yanayohusisha usanifu, ukataji wa vyuma, injini 2 na majenereta 3 yamefikia asilimia 35 na kwamba makontena 300 yenye vifaa hivyo yatawasili nchini Septemba 2019 kutoka nchini Korea.
Baada ya kukagua hali ya meli ya Mv Victoria na Mv Butiama ambazo ukarabati wake umeanza, Rais Magufuli namewasalimu wafanyakazi walioajiriwa katika mradi huo na kuwaagiza wakandarasi kuhakikisha wanalinda maslahi yao na sheria za usalama kazini kuzingatiwa.
Pia Rais Magufuli ameagiza mitambo miwili ya kunyanyulia mizigo (Cranes) iliyokuwa imeuzwa na Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) kurejeshwa mara moja.
Wakati huo huo, Rais Magufuli amefanya ziara ya kushtukiza katika Gereza Kuu la Butimba Jijini Mwanza ambapo amezungumza na wafungwa na Askari Magereza.
Wafungwa wa gereza hilo wamemueleza kero mbalimbali wanazokabiliana nazo na pia Askari Magereza wamemueleza changamoto mbalimbali ambazo ameahidi kuzifanyia kazi.
Akiwa njiani kutoka Butimba, Rais Magufuli amesimama na kuwasalimu wananchi waliokuwa wamekusanyika kwa maelfu katika eneo hilo na baada ya kuelezwa kero ya kukosekana kwa wodi ya wanaume katika Hospitali ya Wilaya ya Ilemela amemuagiza Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza kuhakikisha jengo la wodi hiyo ambalo limetengewa shilingi Milioni 300 linakamilika ifikapo tarehe 30 Julai, 2019.

VIDEO: RAIS MAGUFULI ATOA NG’OMBE WATATU KWA WAFUNGWA WA GEREZA LA BUTIMBA

Rais John Magufuli leo Jumanne Julai 16, 2019 ametembelea Gereza la Butimba mkoani Mwanza ambapo amepata fursa ya kuzungumza na wafungwa na maofisa wa gereza waliotoa kero zao, akiwa katika Gereza la Butimba amewaahidi wafungwa na maofisa wa gereza hilo kuwapatia ng’ombe watatu na magunia 15 ya mchele kwa ajili ya chakula.
“Nimegundua mambo mengi hapa hata mengine hamjaeleza kuna vitendo mnavyofanyiwa hamjavisema ninajua kuwa mnaombwa rushwa hivyo ninaomba muamini nimeona na nimesikia, mvumilie hata sisi tuliopo hapa ni wafungwa au mahabusu wa baadae,”

Akiongea Mfungwa wa miaka 30 Kalikenya Nyamboge ameyasema haya:-
“Mheshimiwa Rais kuna Ofisa Usalama yuko huku ndani ana anawapa wafungwa simu halafu zikikamatwa tunanyan’ganywa vitu vyetu lakini hadi leo hajafanywa kitu chochote,”

“Mheshimiwa rais huyu Ofisa akupe mihuri na hizo simu uondoke nazo utajua mwenyewe utaenda kufanyia nini na ikibidi ondoka naye kwani ukifanya hivyo utakiwa umetusaidia sana na ukimuacha atanidhuru,”

“Sasa hivi Jenerali Kamishna ametuletea daktari msomi na alivyofika vifo ndiyo vimepungua maana walikua wakikuchoma sindano wanakuua,”-  alisema Mfungwa Kalikenya

Msekwa: Tumepokea barua ya Makamba, Kinana

KATIBU wa Baraza la Ushauri la Viongozi Wakuu Wastaafu wa CCM, Pius Msekwa, amesema wanasubiri vikao vya chama hicho tawala kuamua juu ya kile kilichoandikwa katika barua ya malalamiko ya makatibu wakuu wawili wastaafu, kwamba wamedhalilishwa kwa mambo ya uzushi na uongo.
Juzi, makatibu wakuu hao wawili wastaafu wa CCM, Yusuf Makamba na Abdulrahman Kinana, walimwandikia barua Msekwa wakilalamika kudhalilishwa kwa mambo ya uongo na mtu anayejitambulisha kama mwanaharakati na mtetezi wa Serikali.
Akizungumza na MTANZANIA jana, Msekwa alisema tayari barua ya malalamiko ya wastaafu hao imewafikia na kwamba nyingine kama hiyo pia ilifikishwa kwa Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. John Magufuli na Katibu Mkuu, Dk. Bashiru Ally.
Msekwa ambaye alisema barua hiyo ambayo ni ya kwanza kuwafikia wao kama Baraza la Wazee Wastaafu, kwa kawaida itapelekwa kwenye chama hicho ambacho ndicho kinachopaswa kuitisha vikao kushughulikia malalamiko yaliyotajwa.
“Hii ni mara ya kwanza kupokea malalamiko ya aina hii, kwanza hakuna utaratibu wa kawaida, lakini tutafuata taratibu za chama, tutapeleka kwenye chama chenyewe.
“Barua hii nakala yake imeenda pia kwa Mwenyekiti wa chama na Katibu Mkuu. Hivyo sisi kama Baraza la Wazee tunasubiri utaratibu wa chama kwanza,” alisema Msekwa.
Alipoulizwa kwanini wakiwa kama Baraza la Wazee hawajakemea mambo hayo kabla hata hawajapelekewa barua, Msekwa alisema kwa mujibu wa Katiba ya CCM kazi yao ni kutoa ushauri.
Katika hilo, Msekwa ambaye amepata pia kuwa Spika wa Bunge, alisema ushauri hautolewi kama amri bali unaombwa.
Jana gazeti hili lilimtafuta Dk. Bashiru mara kadhaa kupitia simu ya mkononi, lakini hakupokea wala kujibu ujumbe mfupi wa maneno aliotumiwa.
Akihojiwa jana na kipindi cha ‘Power Breakfast’ kinachorushwa na kituo cha redio cha Clouds FM, kuhusu ufafanuzi wa barua hiyo, Makamba alimtaka mtangazaji alisome tamko lao kwa sababu linajitosheleza.
“Soma hilo tamko linajitosheleza soma. Je, unalo? Hili tamko halifai kuondolewa koma wala nukta, linatakiwa libaki kama lilivyo, ni tamko refu, ni zuri, tumeliandika vizuri, tumeliandika mimi na rafiki yangu Kinana, halitakiwi kuongezwa kitu, libaki kama lilivyo,” alisema.
Alipoulizwa tamko hilo lina maana gani, Makamba alimwambia mtangazaji; “Wala usiulize, utakapolisoma utalielewa, mbona una haraka? Tafuta, usiwe na haraka.”
Baada ya majibishano hayo, mtangazaji huyo alimwuliza Makamba kama huwa wanaonana mara kwa mara na Kinana na alijibu; “Usitake tena maneno ya umbea kutoka kwangu soma tamko.”
Makamba na Kinana waliopata kushika nafasi ya ukatibu mkuu wa CCM kwa kufuatana wakati wa Serikali ya awamu ya nne, walitoa taarifa ya maandishi kwa umma juzi, huku wakiweka bayana kwamba wamezingatia Katiba ya CCM toleo la mwaka 2017 ibara ya 122.
“Tumewasilisha maombi yetu tukiwasihi wazee wetu watumie busara zao katika kushughulikia jambo hili ambalo linaelekea kuhatarisha umoja, mshikamano na utulivu ndani na nje ya chama.
“Mara kadhaa ametutuhumu sisi wawili, makatibu wakuu wastaafu wa CCM kwa mambo ya uzushi na uongo,” walisema katika barua hiyo.
Vilevile walisema wametafakari kwa kina kabla ya kutoa taarifa kuhusu taarifa wanazodai za uzushi kwa nyakati mbili tofauti.
Walisema kwa sasa Watanzania wanajua kuwa yanayosemwa na mtu huyo si ya kwake.
Kwamba mara kwa mara Watanzania wamekuwa wakijiuliza kwamba mtu huyo (wamemtaja, lakini jina lake tunalihifadhi kwa sababu za kitaaluma) anatumwa na nani.
“Pili anakingiwa kifua na nani? Tatu anatumika kwa malengo gani? Na nne nini hatima ya mikakati yote hii.
“Tafakari yetu inatupeleka kupata majibu yafuatayo; kwanza kwa ushahidi wa kimazingira mtu huyu anatumwa na kutumiwa na watu wenye uwezo wa kumlinda na kumkingia kifua bila kuhojiwa na taasisi yoyote wala mtu yeyote.
“Pili zipo ishara kwamba watu hawa wanaomkingia kifua wana mamlaka, baraka na kinga ambazo wamepewa ili kutekeleza majukumu maalumu kwa watu maalumu na kwa malengo maovu,” walisema katika barua hiyo.
Katika hoja yao ya tatu, walisema mtu huyo anatumika kwa malengo ya kuwazushia, kuwakejeli, kuwavunjia heshima, kuwatia hofu na kuwanyamazisha viongozi, taasisi na watu ambao ni walengwa waliokusudiwa.
“Nne, kuna kila dalili kuwa lengo na hatima ya mkakati huu ni kuandaa tufani ya kuwahusisha walengwa, wastaafu na walio kazini katika nafasi mbalimbali na matendo ya kihalifu, kimaadili na kihaini ili kuhalalisha hayo wanayokusudia kuyafanya.
“Tumeamua kutochukua hatua za kisheria kwa sasa kwa sababu kwanza jambo hili lina taswira ya kimkakati na lina mtandao wenye malengo ya kisiasa. Kwa hiyo linapaswa kushughulikiwa kisiasa.
“Pili, unapochafuliwa, unachokwenda kudai mahakamani ni fidia. Kwetu sisi, heshima yetu haiwezi kuthaminishwa na fidia,” walisema.
Wakizungumzia kuhusu chanzo cha tuhuma hizo, wazee hao walisema wanaamini kuna sehemu zinatoka.
“Yeye anatumwa kutekeleza maagizo na kutumika kama kipaza sauti tu. Huyu ni mamluki anayetumika kuivuruga CCM na nchi yetu. Katika mazingira hayo, hatuwezi kukaa kimya.
“Baada ya kupata ushauri kutoka kwa watu mbalimbali, wakiwemo viongozi wakuu wastaafu wa CCM, viongozi wa dini, wanataaluma, wanahabari, wana-CCM na wananchi kadhaa, tumeamua kutoa tamko kuhusu uzushi anaojitahidi kuueneza,” walisema katika taarifa hiyo.
Aidha walisema mara ya kwanza walizushiwa kwamba wanamkwamisha Rais John Magufuli kutekeleza majukumu yake.
“Tuliyapuuza haya, kwanza kwa imani kwamba viongozi wetu watayaona kwa namna yalivyo kuwa haiwezekani tushiriki kuihujumu Serikali ya chama tulichokitumikia maisha yetu yote.
“Haiingii akilini kwamba wastaafu wawili walio majumbani mwao, wana uwezo wa kumzuia Rais, Amiri Jeshi Mkuu na mwenyekiti wa chama kutekeleza majukumu yake,” ilisema taarifa hiyo.
Walisema kwa mara ya pili wamezushiwa tuhuma nyingine kwamba wanataka kumhujumu Rais ili asipitishwe na CCM kutetea urais mwaka 2020.
“Katika utumishi wetu, tumesimamia michakato ya kupitisha wagombea wa nafasi ya urais na nyinginezo na kwamba tuhuma hizo ni uzushi uliosukwa kwa malengo maalumu na kwamba msingi wa tuhuma zote mbili ni hofu.
“Tuliamini kabisa kwamba pale anapojitokeza mtu hadharani na kuwadhalilisha viongozi waandamizi wastaafu na huku mtu huyo akijinasibisha na Serikali pamoja na Rais ambaye ni mwenyekiti wa CCM, basi hatua zitachukuliwa na taarifa kutolewa kwa umma,” inasomeka taarifa hiyo.

JPM kuwasha moto kwa waliotibiwa Mafua India

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amemuagiza Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu, kuhakikisha anafuatilia malipo yote ambayo Serikali inatakiwa kulipa Nchini India.

Rais Magufuli ameyabainisha hayo jana Julai 15, wakati wa shughuli ya uzinduzi wa Huduma za Tiba katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando, ambapo amesema lengo la kufanya hivyo, ni kudhibiti  vizuri matumizi ya watu wanaotibiwa India ilihali hawana magonjwa ya kuwapeleka huko.
''Wapo watu hapa waliokuwa wanapewa vibali kwenda kutibiwa India kumbe wanaumwa mafua, Mh Waziri  wa Afya akafuatilie malipo tunayotakiwa kulipa India, ukikuta kuna mtu alitibiwa wakati hakuwa mgonjwa akazilipe mwenyewe, lazima tujenge nidhamu ya nchi yetu'' amesema Rais Magufuli.
Aidha Rais Magufuli ameongeza kuwa, Serikali haikatai watu kwenda kutibiwa nje, lakini iwe ni kwa magonjwa, ambayo yameshindikana kutibika hapa nchini.
Rais Magufuli pia imeitaka Wizara ya Afya, kuhakikisha lazima inapata ufumbuzi wa kweli, ili kubaini nini chanzo na sababu inayopelekea, wananchi na wakazi wa kanda ya Ziwa kuongoza  kwa kuumwa ugonjwa wa Saratani.

Saturday, July 13, 2019

Chris Brown aanza kumfuatilia Vanessa Mdee

Baada ya mwimbaji wa miondoko ya RnB Chris Brown kutangza kolabo yake na mkali wa Nigeria Davido Ijumaa ya July 12,2019 sasa huenda kukawa kuna nyingine kutokea hapa nyumbani hii ni baada ya CB kuonekana kum-follow Vanessa Mdee kwenye instagram yake.
Vanessa Mdee amekuwa miongoni mwa wafuasi zaidi ya Elf 3 ambao Chris Brownanawa-follow kupitia ukurasa wake wa instagram, mashabiki wengi wameibuka na kudai kuwa huenda CB amevutiwa na uwezo wa Vee kwenye masuala ya muziki.
Inawezekana kuwa Vanessa Mdee ndio msanii wa kwanza wa kike Afrika Mashariki kuwa miongoni mwa wafuasi wa CB, kupitia Insta story Vanessa hakutaka kuificha good news hii alipost na kuandika ‘Nina uhakika kuwa wote mnafahamu kuwa nampenda huyu kijana, Chris Brown anani-follow”

Friday, July 12, 2019

Whozu ajibu kuhusu kufanya mapenzi kwenye gari

Msanii wa muziki wa kizazi kipya hapa nchini Tanzania Whozu "Dingoo", amefunguka kuwa ameshawahi kuazima magari ila hajawahi kufanya mapenzi kwenye gari.


Whozu amesema hayo wakati alipofanya mahojiano na EATV & EA Radio Digital, baada ya kuulizwa suala la yeye kuazima gari pamoja na swali la kizushi kama aliwahi kufanya mapenzi kwenye gari haswa baada ya kutamba sana baada kununua gari yake.
"Huo utoto wa kufanya mapenzi kwenye gari sijawahi kufanya, nilishaazima gari kitambo, niliazima tu kwa michongo ya hapa na pale kipindi ambacho sina gari, lakini kwa sasa hivi Mungu kanijaalia uwezo wa kuwa na gari yangu, kuwa na maisha yangu, muziki wangu na mashabiki zangu wananipokea".
Pia Whozu amefunguka kuhusu kauli ya Dogo Janja ambaye aliwahi kusema wasanii wapya hakuna na waliopo wanapungua kwa kusema, ''Janjaro ni mtu wa utani sana, ni mtu ambaye anaandika caption nzuri lakini sio kila muda yupo seriazi sana''.

Thursday, July 11, 2019

RAIS MAGUFULI "KASIMU KANGU KAKIMEO, KATA HELA POPOTE WALA SIKUOMBI"

Bonyeza play hapa chini kutazama zaidi pia tembelea app hii kila Mara kusoma habari mpya

Kabudi akanusha taarifa ya Azory Gwanda kufariki

Waziri wa Mambo ya Nje Palamagamba Kabudi, amesema hajathibitisha kuwa aliyekuwa mwandishi wa habari za uchunguzi wa gazeti la Mwananchi Azory Gwanda, kuwa amefariki Dunia na kueleza mpaka sasa vyombo vya ulinzi na usalama vinaendelea kuanya uchunguzi.


Waziri Kabudi ametoa kauli hiyo akiwa Uingereza kwenye mkutano wa nchi za Jumuiya ya Madola ambao unalenga kujadili ya hali ya utawala bora, katia nchi hizo.
Akizungumza nchini Uingereza Kabudi amesema kuwa "mpaka sasa hakuna uthibitisho kuwa Azory yuko hai au amefariki, vyombo vya ulinzi na usalama vinaendelea kuchunguza tukio hilo na matukio mengine, yaliyotokea katika machafuko ya Kibiti."
Aidha amesema kuwa "kuhusu kile nilichokisema, katika mahojiano yangu BBC , nilieleza kuwa tukio lililotokea Kibiti lilikuwa la kuhuzunisha, na wapo Watanzania waliouawa na wengine kupotea, sikuthibitisha kuwa Azory Gwanda amefariki."
Mapema Julai 11, 2019, wakati akifanya mahojiano maalum kuhusiana ahali ya usalama Tanzania kwenye kituo cha habari cha BBC Waziri Kabudi alisema kuwa "tatizo la Rufiji ni moja ya matukio yaliyoumiza na kusikitisha ambayo TZ tumeyapitia, pale Rufiji sio Azory Gwanda pekee ambaye amepotea na kufariki,nikuhakikishie tunachukua kila hatua, ili watu wetu wawe salama awe Mwanahabari,Polisi au raia wa kawaida."

"Anayetaka kuwashtaki, anishtaki mimi" - Makonda

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda ameanza maandalizi kuelekea mkutano mkuu wa nchi za SADC, unaotarajia kufanyika Agosti 2019 jijini Dar es salaam, ambapo leo amekutana na waendeshaji wa mitandao ya kijamii na kuwakabidhi maswali 12,


kwa ajili ya kuwauliza wananchi kuelekea mkutano huo.
Makonda amefikia maamuzi hayo leo jijini Dar es salaam, ambapo ameeleza lengo la mkakati huo, ni kuhakikisha wananchi wanakuwa na uelewa kuhusiana na mkutano wa SADC, pamoja na kujua kiundani juu ya umuhimu wa mkutano huo kwenye masuala ya biashara.
Makonda amesema kuwa "tufanye jambo litakalotikisa Mkoa wetu, nataka tufanye mashindano yatakayokuwa na zawadi, zawadi ya kwanza itakuwa wewe na kamera yako, na zawadi ya pili itaenda kwa mwananchi utakayefanya naye kazi."
"Nataka siku ya kutoa zawadi iwe tarehe 5 Agosti 2019, nataka kwa yeyote mwenye Platform, asaidie kupatikana kwa majibu ya maswali 12, na mwisho wa siku atajichukulia milioni 3." ameongeza Makonda
Aidha Makonda kuhusiana na ugumu wa kufanya kazi hiyo amesema kuwa "SADC kuna kila kitu,pia hii ni kazi ya Serikali hakuna wa kukuhoji,muifanye kwa moyo mkunjufu bila hofu, kama mtu atakushtaki aanze kunshtaki mimi. "

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Yavitaka Vyama vya Siasa Viache Kupeleka Malalamiko Katika Vyombo vya Habari

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imevitaka vyama vya siasa nchini kutopeleka malalamiko yao katika vyombo vya habari kuhusu masuala ya uchaguzi na badala yake viwasilishe hoja hizo katika Kamati za Maadili za Uchaguzi.

Imesema haina mfumo wa kushughulikia malalamiko ya uchaguzi kupitia vyombo vya habari badala yake imetaka utaratibu wa kisheria kufuatwa ili haki itendeke kwa wote. 

Mkurugenzi wa NEC, Dk Athuman Kihamia alisema hayo akiwasilisha mada ya Uboreshaji daftari la kudumu la wapigakura katika semina ya viongozi wa vyama vya siasa, dini, walemavu, vijana, wanawake, asasi za kiraia na watendaji wa NEC.

‘’Pamoja na uwepo wa Kamati za maadili zenye mamlaka ya kutatua migogoro na kuweka mazingira sawa ya ushindani katika chaguzi ndogo, vyama vimekuwa havipeleki malalamiko yao kwenye kamati hizo bali hutoa malalamiko yao kupitia vyombo vya habari, ‘’ alisema. 

Alizitaja kamati zinazoundwa wakati wa uchaguzi kuwa za maadili ya uchaguzi, kamati ya rufaa, kamati ya maadili ya kitaifa, kamati ya maadili ya jimbo na kamati ya maadili ya kata.

Mwenyekiti wa NEC, Jaji mstaafu Semistocles Kaijage alisema kifungu cha 15 (5) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, sura ya 343 kikisomwa na kifungu cha 21 (5) cha Sheria ya uchaguzi ya serikali za mitaa kinaipa NEC mamlaka kuboresha daftari la kudumu la wapigakura.

Alisema pia NEC iliendesha uhakiki wa vituo vya kuandikisha wapigakura nchini ambapo kwa mkoa wa Kilimanjaro, iliongeza vituo vya kujiandikisha kutoka vituo 1,273 hadi 1,286.

Breaking News: Tazama Hapa Matokea Ya Kidato cha Sita 2019

Baraza la Mitihani la Taifa (Necta) nchini Tanzania leo Alhamisi Julai 11, 2019 limetangaza matokeo ya kidato cha sita 2019.

Katika matokeo hayo yaliyotangazwa na Katibu Mtendaji wa Necta mjini Unguja Zanzibar, Dk Charles Msonde amesema ufaulu umeongezeka kutoka asilimia 97.58 mwaka 2018 hadi kufikia asilimia 98.32 mwaka 2019 ikiwa ni sawa na asilimia 0.74.

Dk Msonde amesema mtihani huo uliofanyika kati ya Mei 6 hadi 23 mwaka 2019, watahiniwa 91,298 walisajiliwa wakiwamo wasichana 37,948 sawa na asilimia 41.56 na wavulana 53,350 sawa na asilimia 58.44.

Amesema kati ya watahiniwa waliosajiliwa, watahiniwa wa shule walikuwa 80,216 na watahiniwa wa kujitegemea walikuwa ni 11, 082.

1.Kutazama matokeo ya Kidato cha Sita <<BOFYA HAPA>>.

2.Kutazama Matokeo Ya Mtihani Wa Ualimu 2019  <<BOFYA HAPA>>

DC ashinda kura za maoni jimbo la Lissu

WAJUMBE wa Mkutano Mkuu wa CCM Jimbo la Singida Mashariki, wamepiga kura kupata mwana CCM mmoja ambaye atapeperusha bendera ya chama hicho katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Julai 31.
Katika mkutano huo uliofanyika jana, wanachama 13 walichuana katika uchaguzi huo na Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Miraji Mtaturu, ameongoza kura za maoni kwa kupata kura 396.
Uchaguzi huo unafanyika baada ya aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Tundu Lissu kupoteza sifa.
Mbali ya Mtaturu, wana-CCM wengine waliochuana katika kura hizo za maoni ni pamoja na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Luteni mstaafu Chiku Galawa aliyepata kura 40.
Wengine na kura zao katika nabano ni Thomasi Kitima (79), Martini Lissu (29), Lazaro Msaru (17), Hamisi Maulidi (12),  Mwanahamisi Mujori (7), Mariamu Nkumbi (7), Moris Mukhoty (4), Jeremia Ihonde (4), Sylivester Meda (3), Shilinde Kasure (1) na Emmanuel Hume (1).
Katika uchaguzi huo ambao ulikuwa na utulivu, kila mgombea aliweza kunadi sera zake mbele ya wapigakura na kisha kuulizwa maswali kwa mujibu wa utaratibu uliotangazwa na msimamizi wa uchaguzi huo, Katibu wa Sekreterieti CCM Taifa, Salum Leja.
Leja alisema kuwa wajumbe wa mkutano mkuu wamekamilisha kazi yao ya hatua ya kwanza na sasa kinachofuata majina ya wagombea watatu yatakwenda katika vikao vya ngazi ya juu ya chama.
Akizungumza baada ya kutangazwa kushinda kura za maoni, Mtaturu, alisema kuwa Jimbo la Singida Mashariki limekuwa nyuma kimaendeleo, hivyo pindi atakapoteuliwa na chama chake anaomba ushirikiano na wananchi wote wa Singida Mashariki na Wilaya ya Ikungi kwa ujumla.
“Ninawashukuru wana CCM wenzangu kwa kunipa ushindi mnono na sote tunaona namna jimbo letu lilivyo nyuma kwa maendeleo, na pindi chama kikinipa ridhaa na kuwa mgombea, ninaomba wote tushirikiane ili tuweze kuleta maendeleo,” alisema Mtaturu,
Naye mshindi wa tatu katika kura hizo za maoni, Luteni mstaafu Chiku Galawa, alisema ameridhika na matokeo ya uchaguzi huo na atashirikiana na mwana CCM yeyote ambaye atateuliwa na chama kuweza kusukuma gurudumu la maendeleo katika jimbo hilo.
“Sina kinyongo na nimeridhika kabisa na matokeo haya, kikubwa sasa tushirikiane kwa pamoja ili kuleta maendeleo,” alisema Galawa.
Kwa upande wake Katibu wa CCM Ikungi, Noverty Kibaji alisema wanachama hao baada ya kupigiwa kura za maoni za ndani ya chama, walioshinda nafasi tatu za juu, majina yao yatawasilishwa vikao vya juu kwa uamuzi.
 “Uchaguzi huu umefanyika kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu za chama chetu na tunaamini vikao vya ngazi ya juu ndio vitakuwa na maamuzi nani atakayepeperusha bendera ya chama katika uchaguzi huu wa marudio,” alisema.

Kigwangalla akubali yaishe sanamu la Nyerere

Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt Hamis Kigwangalla , ameomba kupewa muda ili kurekebesha mfano wa sanamu ambalo lilichongwa kuashiria kuwa ni Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere, ambalo hivi karibuni lilizua mjadala mkubwa hususani kwenye mitandao ya kijamii.



Katika uzinduzi wa hifadhi ya Burigi iliyoko Wilaya Chato mkoani Geita Waziri Kigwangala, alimkabidhi Rais Magufuli mfano wa sanamu la Mwalimu Nyerere, huku watu mbalimbali wakidai sanamu hilo halina uhalisia na Mwalimu Nyerere.
Waziri Kigwangalla amesema kuwa "Baba wa Taifa alitoa tamko la kwanza la Uhifadhi nchini, ambalo ndiyo dira yetu, tuache dhihaka kwa sababu hakuna aliyefanya kazi ile kwa kusudi hilo, tumesema linashughulikiwa tunaomba mtuamini, mtupe muda turekebishe."
"Kilichonifurahisha ni kuwa kizazi cha vijana wa kisasa, bado kinamkumbuka vizuri Baba wa Taifa, kinamuenzi na kumheshimu sana, ndiyo maana wanaikumbuka taswira yake, tutatumia vizuri zaidi wataalamu wetu kurekebisha mapungufu yaliyojitokeza kabla ya kuitumia" ameongeza Kigwangalla
Hivi karibuni kwenye uzinduzi wa hifadhi ya Burigi Waziri Kigwangalla alimkabidhi tuzo maalum ambayo hifadhi ya Taifa ya Serengeti ilishinda kwa ni hifadhi bora barani Afrika.
Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list