Rais John Magufuli leo Jumanne Julai 16, 2019 ametembelea Gereza la Butimba mkoani Mwanza ambapo amepata fursa ya kuzungumza na wafungwa na maofisa wa gereza waliotoa kero zao, akiwa katika Gereza la Butimba amewaahidi wafungwa na maofisa wa gereza hilo kuwapatia ng’ombe watatu na magunia 15 ya mchele kwa ajili ya chakula.
“Nimegundua mambo mengi hapa hata mengine hamjaeleza kuna vitendo mnavyofanyiwa hamjavisema ninajua kuwa mnaombwa rushwa hivyo ninaomba muamini nimeona na nimesikia, mvumilie hata sisi tuliopo hapa ni wafungwa au mahabusu wa baadae,”
Akiongea Mfungwa wa miaka 30 Kalikenya Nyamboge ameyasema haya:-
“Mheshimiwa Rais kuna Ofisa Usalama yuko huku ndani ana anawapa wafungwa simu halafu zikikamatwa tunanyan’ganywa vitu vyetu lakini hadi leo hajafanywa kitu chochote,”
“Mheshimiwa rais huyu Ofisa akupe mihuri na hizo simu uondoke nazo utajua mwenyewe utaenda kufanyia nini na ikibidi ondoka naye kwani ukifanya hivyo utakiwa umetusaidia sana na ukimuacha atanidhuru,”
“Sasa hivi Jenerali Kamishna ametuletea daktari msomi na alivyofika vifo ndiyo vimepungua maana walikua wakikuchoma sindano wanakuua,”- alisema Mfungwa Kalikenya


No comments:
Post a Comment