Na.Enock Magali,DODOMA
SERIKALI imeitaka mifuko ya Uwezeshaji wananchi kiuchumi pamoja na Taasisi za kifedha nchini kuwaunga mkono kwa kuwawezesha kimitaji wawekezaji Vijana ambao wamedhamiria kujiajiri na kuajiri Vijana wengine.
Hayo yamesemwa July 10 Jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Kazi,Ajira,Vijana na Watu wenye Ulemavu Mh.Antony Mavunde alipotembelea katika Kiwanda cha Nguo cha Vinceberg Garments Co. Ltd kinachomilikiwa na Bi Doreen Mringi ambapo alitumia fursa hiyo kupongeza uwekezaji huo na kuitaka Mifuko yenye dhamana ya kuwezesha wananchi kiuchumi imfikie na kumumsaidia kukua kimtaji.
Pamoja na hayo Mh Mavunde alishangazwa na ubora wa jezi na T.shirts zinazotengenezwa na Vijana wa Kitanzania katika kiwanda hicho.
"Kiwanda hichi kimetoa Ajira 70 kwa Vijana wa Kitanzania na imani yetu ni kwamba utazalisha Ajira zaidi ukiongeza upanuzi wa kiwanda hichi,kama Serikali lazima tukusaidie kufikia malengo hayo kwa kuhakikisha unapata fursa ya uwezeshwaji mtaji kupitia mikopo inayotolewa kwa Wawekezaji kupitia mifuko mbalimbali ya uwezeshwaji wananchi kiuchumi"Alisema Mavunde.





No comments:
Post a Comment