Baraza la Wazee la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), limeitaka serikali kurejea ahadi yake ya kumalizia mchakato wa katiba mpya iliyoitoa mwaka 2015 wakati wa uchaguzi mkuu.
Wazee hao wamedai kuwa mchakato huo bado una umuhimu mkubwa kwa Watanzania.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Baraza hilo, Hashim Juma Issa, alidai kushangazwa na ukimya wa serikali kuhusu mchakato huo ambao uligharimu fedha nyingi za Watanzania.
Wazee hao wanadai kusitishwa kwa mchakato huo ni hasara kubwa kwa Taifa kwa kuwa mchakato huo ulishaanza na umegharimu fedha nyingi, hivyo kutaka uendelezwe kwa maslahi ya Taifa.
Katika hatua nyingine, wazee hao wamelalamikia kuingiliwa kwa mikutano ya wabunge wa chama hicho na Jeshi la Polisi, wakidai kitendo hiko ni ukiukwaji wa misingi ya demokrasia nchini na kounya kuwa vitendo hivyo vinaweza kupelekea uvunjifu wa amani.
Kuhusu uchaguzi wa serikali za mitaa, wameapa kulinda kura kwa madai ya kuchoka kuibiwa kura kila uchaguzi unapofika, na kulionya Jeshi la Polisi kuwa waangalifu katika uchaguzi huo ili kuepusha uvunjifu wa amani.
No comments:
Post a Comment