CEO wa Simba Senzo Mazingiza amekuja na mkakati ambao utaiwezesha klabu hiyo kupunguza matumizi yasiyo ya lazima
Senzo aliyeingia ofisini mwezi uliopita akichukua nafasi ya Crescentius Magori ambaye mkataba wake ulimalizika, ameweka mkakati huo baada ya kutoridhishwa gharama ambazo Simba imekuwa ikitumia
Moja ya mambo ambayo ameyafanyia kazi kwa haraka, ni kukamilika kwa ujenzi wa uwanja wa Simba ulioko Bunju jijini Dar es salaam
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Mohammed Dewji tayari ameahidi Simba huenda ikaanza kufanya mazoezi kwenye uwanja huo kuanzia mwishoni mwa mwezi huu
Simba imekuwa ikitumia uwanja wa Gymkhana kwa ajili ya mazoezi ambao gharama yake kwa siku ni Tsh 500,000/-. Wakati mwingine hutumia uwanja wa Boko Veterans ambao gharama yake sio chini ya 300,000/-
Pia inaelezwa Senzo amehamisha kambi ya Simba iliyokuwa ikiwekwa Sea Scape Hotel
Bosi huyo ameahidi kufuatilia kwa ukaribu michakato ya usajili iliyofanyika
Ameeleza kushangazwa na Simba kusajili wachezaji kutoka Brazil
No comments:
Post a Comment