Mbunge wa Jimbo la Kinondoni,Abdallah Mtolea, amewatia moyo wale wote wanaolalamika kuhusu hali ngumu, kwakuwa ugumu wa maisha ndiyo kipimo cha maendeleo kwa mtu na kwamba hakuna nchi yoyote ambayo ilishawahi kuendelea bila kupitia nyakati ngumu
Mbunge Mtolea ametoa kauli hiyo, wakati akizungumza kwenye kipindi cha East Africa BreakFast cha East Africa Radio, ambapo amekiri kuwa hali ni ngumu na kuwataka wananchi wawe wavumilivu.
"Wengi wanasema hali ni ngumu ila niwaambie, hakuna nchi ambayo iliendelea kwenye hali ambayo ni nyepesi, lazima tupate maendeleo kwenye hali ngumu." amesema Mtolea.
Aidha akizungumzia suala la kuhama chama, Mtolea amesema kuwa hana mpango huo na ataendelea kuwa ndani ya Chama Cha Mapinduzi.
''2020 nitaendelea kuwa Chama Cha Mapinduzi, uzuri ukiwa CCM ukienda kwa kiongozi wa Serikali unakuwa kama umeenda kwa Baba, yaani ndiyo maana kila kitu kinaenda kiurahisi'' amesema Mtolea.
No comments:
Post a Comment