Mbunge wa CCM kutoka jimbo la Temeke, Abdallah Mtolea, amesema kwa sasa hawezi kumshauri chochote, aliyekuwa Wakili wa kujitegemea Fatma Karume juu ya chama gani cha siasa ambacho anaweza kujiunga nacho kwa sasa endapo atatangaza kujiingia kwenye siasa.
Mbunge Mtolea ametoa kauli hiyo wakati akizungumza kwenye kipindi cha Kikaangoni kinachoruka kupitia kwenye kurasa za Facebook na Youtube ya EATV, ambapo amesema anaweza kumshauri Fatma Karume chama cha kwenda endapo atamfuata na kujua malengo yake.
"Kuhusu Fatma Karume kusimamishwa Uwakili Tanzania Bara, kwenye sheria tunafundishwa kukubaliana na hukumu yeyote inayotolewa, ila kama hujakubaliana nayo huwezi kusema hadharani kwamba hukubaliani nayo, kuhusu kumshauri kwa sasa ajiunge chama gani siwezi kumshauri kwanza sijui anataka kwenda kufanya nini kwenye siasa" amesema Mtolea
"Kama akija kwangu nitamsikiliza anataka kufanya nini na anataka kwenda kugombea au lah unajua si kila mwanasiasa anataka kuingia kwenye siasa anataka kuwa kiongozi, lazima nijue anataka kwenda wapi kama anataka kuwa mkosoaji wa Serikali, nitamueleza chama cha kwenda" amesema Mbunge Mtolea
No comments:
Post a Comment