Simba imeendeleza moto wa ushindi ligi kuu ya Vodacom baada ya kuichapa Biashara United mabao 2-0 katika mchezo uliopigwa uwanja wa Karume, Musoma
Huo ulikuwa ushindi wa nne mfululizo kwa Simba ambayo imejikita kileleni mwa msimamo wa ligi baada ya kufikisha alama 12
Meddie Kagere 'Terminator' bado hazuiliki akifunga bao lake la sita msimu huu
Kagere amefunga katika michezo yote minne
Miraji Athumani nae ameshajenga utamaduni wa kutupia kambani kila anapotaka, akifunga bao lake la tatu msimu huu akiutendea haki mpira wa adhabu uliopigwa na Ibrahim Ajib
Ulikuwa ni mchezo ambao Simba waliutawala kiufundi zaidi
Kocha Patrick Aussems ameendelea kuonyesha umahiri kwa kufanya mabadiliko ya kikosi kulingana na mchezo husika
No comments:
Post a Comment