Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimetoa maoni yake juu ya Mkurugenzi mpya wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Dkt Wilson Charles, na kwamba kwa sasa wamejipanga kushughulika naye kuelekea katika Uchaguzi Mkuu ujao.
Akizungumza na EATV&EA Radio Digital leo Oktoba 1, 2019, Mkurugenzi wa Mawasiliano, Itifaki na Mambo ya Nje wa chama hicho John Mrema, amesema kwa sasa hawezi kumzungumzia Mkurugenzi aliyepita na badala yake wanamtakia heri na fanaka kwa majukumu yake mengine.
"Aliyepita ameshapita, kwa hiyo hata tukimzungumzia haisaidii, tumtakie kila la heri huko anakoenda kupangiwa kazi nyingine, tushughulike tu na huyu ambaye yupo na tutakayekuwa naye kwenye uchaguzi muda mchache ujao" amesema Mrema.
Mara kwa mara chama hicho kilikuwa kikiingia kwenye migogoro na aliyekuwa Mkurugenzi wa NEC Dkt Athuman Kihamia.
TUMEBORESHA APP YETU, TAFADHALI BOFYA HAPA CHINI KUDOWNLOAD APP YETU MPYA ILI KUENDELEA KUPOKEA HABARI KWA WAKATI NA KUTAZAMA MECHI ZOTE LIVE ( UKISHA BOFYA, BONYEZA NENO OPEN IN PLAY STORE KISHA INSTALL )
BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YETU MPYA BURE KABISA
No comments:
Post a Comment