We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Tuesday, October 1, 2019

Yanga yaanza kumnyatia Mshambuliaji huyu wa UD SONGO

Unamkumbuka yuke mshambuliaji wa UD Songo aliyewafunga Simba walipokuja kucheza jijini Dar es salaam?
Anaitwa Luís Miquisson, taarifa zinaeleza yuko kwenye rada za Yanga
Baada ya safu ya ushambuliaji ya Yanga kuanza kwa kusuasua, imeelezwa mchakato wa kusaka washambuliaji ili kuiongezea nguvu safu hiyo umeanza
Mwenyekiti wa Yanga Dk Mshindi Msolla ameeleza kuvutiwa na mshambuliaji huyo na amekiri kutuma watu wamfuatilie
"Wachezaji tulionao si wabaya sana, tatizo tulilonalo tumeingiza wachezaji wengi wapya, wanahitaji muda wa kukaa pamoja kwa muda mrefu…kwanza hata kwa timu ilivyo sasa, mwalimu Zahera (Mwinyi), amejitahidi sana," Dk Msolla amenukuliwa na gazeti la Bingwa
"Pamoja na hilo, tunahitaji kupata wachezaji wa kiwango cha juu zaidi wa kuamua matokeo…mchezaji kama yule wa UD Songo (Miquissone) ambaye shughuli yake sote tuliiona walipocheza na Simba. Ukiwa na wachezaji wawili au watatu kama wale, unakuwa na uhakika wa ushindi."
Alipoulizwa iwapo Miquissone yupo katika mipango ya Yanga, Dk. Msolla alisema:
"Ndiyo, kuna mtu analishughulikia hilo, lakini pia tunaendelea kuwafuatilia wengine wenye kiwango cha juu kutoka katika timu hizi zilizopo Ligi ya Mabingwa, tutaangalia wale watakaong’ara hatua za awali na raundi ya kwanza kabla ya kuingia makundi"
Pamoja na Luis, Yanga pia huenda ikajaribu kumuwania mshambuliaji wa Platinum FC Perfect Chikwende ambaye juzi aliiangamiza UD Songo kwa kufunga hat-trik kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa na kuipeleka timu hiyo hatua ya makundi
Hata hivyo Yanga haitaweza kumpata mchezaji huyo wakati huu labda mpaka mwezi Juni wakati wa dirisha kubwa la usajili

TUMEBORESHA APP YETU, TAFADHALI BOFYA HAPA CHINI KUDOWNLOAD APP YETU MPYA ILI KUENDELEA KUPOKEA HABARI KWA WAKATI NA KUTAZAMA MECHI ZOTE LIVE ( UKISHA BOFYA, BONYEZA NENO OPEN IN PLAY STORE KISHA INSTALL )

BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YETU MPYA BURE KABISA

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list