Mbunge wa Chambani, Yussuf Salim Hussein (CUF) ameiomba Serikali iongezee fedha Wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi, ili iweze kupanga mipango ya ardhi kwa ajili ya kizazi cha baadae
Hussein ametoa kauli hiyo leo Mei 31, bungeni wakati akichangia Mjadala wa Wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa mwaka 2019-2020.
“Wizara ya ardhi ndio inayobeba maisha yetu,Wizara hii inajukumu kubwa sana,ardhi haiongezeki lakini idadi ya Watanzania na mifugo inaongezeka mahitaji ya vitu vilivyopo juu ya ardhi inaongezeka lazima tuishauri ili tuwe na kilimo cha kisasa.
“Tujenge picha ya miaka 50 ijayo ambayo Watanzania wanaweza kufikia idadi ya watu milioni 100 itakuwaje, lazima Wizara iwezeshwe kupewa fedha ili ipange mipango ya ardhi.
“Tukiangalia miaka mitano au kumi tutaiachia matatizo makubwa kizazi chetu.Tuiombe Wizara itoe fedha nasema haya ndani ya mwezi huu mtukufu wa Ramadhan vinginevyo tutajikuta katika hasara kubwa,”alisema Mbunge huyo.
Pia Mbunge huyo alidai kwamba migogoro ya ardhi inatokana na kutokupimwa kwa maeneo hivyo akaiomba Wizara hiyo ijitahidi ipime maeneo yote .
“Migogoro yote ni kutokana na kutokupimwa kwa maeneo, haya maeneo yanatakiwa yapimwe, yapimwe yote.Tuiombe Serikali kila aliyepewa ardhi basi aitumie na kama haitumii wapewe ambao wanaweza kuitumia,”alisema Mbunge.
No comments:
Post a Comment