Yanga inamuwania mshambuliaji wa Alliance Fc Mapinduzi Balama ili kumuongeza katika kikosi cha mabingwa hao wa kihistoria
Inaelezwa tayari makubaliano baina ya Yanga na mkali huyo wa kutupia mabao yamefikiwa
Hata hivyo kikwazo kimebaki kwa uongozi wa Alliance Fc ambao umetaka kukaa mezani na Yanga wakidai mchezaji huyo bado ana mkataba wa mwaka mmoja
Kumekuwa na utata juu ya mkataba wa mshambuliaji huyo ambapo msemaji wa Alliance Fc Jackson Mwafulango amesisitiza kuwa mkataba wake kunako klabu hiyo bado haujamalizika na ameitaka Yanga kufuata taratibu kama inamtaka
No comments:
Post a Comment