Ikiwa ni miezi miwili tu imepita tangu shirika la ndege la Ethiopian Airlines ndege yake ya Boeing 737 MAX kuanguka, Bado mzimu wa ajali unaendelea kulikumba shirika hilo kwani imeripotiwa kuwa juzi Jumatano usiku ndege moja ya shirika hilo imeponea chupu chupu kuanguka Jijini Lagos nchini Nigeria, baada ya kushindwa kutua mara tatu katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Murtala Muhammed.
Shirika hilo la ndege limethibitisha taarifa hizo na kuydai kuwa ndege hiyo ni Boeing 777-300 na ilikuwa inatoka Addis Ababa na ilishindwa kutua kwa zaidi ya mara tatu kutokana na hali ya hewa kuwa mbaya jambo lililopelekea ndege hiyo kutotua katika uwanja huo.
Ndege hiyo iliyokuwa na abiria wapatao 394, imeelezwa kuwa alikuwemo Rais Mstaafu wa Nigeria, Mzee Olusegun Obasanjo ambaye alikuwa akitokea nchini Ethiopia.
No comments:
Post a Comment