Na. Enock Magali, Dodoma.
Serikali imewaasa vijana wanaohitimu vyuo mbalimbali nchini kutumia elimu wanayoipata kama nyenzo ya kupambana na changamoto ikiwa ni pamoja na kujiajiri.
Rai hiyo imetolewa hii leo na Naibu waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,Mh.William Ole Nasha wakati akifunga maonyesho ya kwanza ya elimu ya Mafunzo na Ufundi yenye dhima ya elimu ya Ufundi na Mafunzo Kwa manufaa ya uchumi wa viwanda, yaliyodumu kwa siku Tano, ambapo wananchi wamepata fursa ya kutembelea na kujifunza dhana mbalimbali.
Ameongeza kuwa,imefika wakati wa vijana wa kitanzania kuondokana na dhana ya kusubiri ajira mara wanapohitimu masomo yao badala yake wafikiria katika kujiajiri mara baaada ya kuhitimu.
"Kumekuwepo na dhana ya wahitimu kuamini kuwa elimu wanayoipata ni kwa ajili ya kupata ajira hasa serikalini na si vinginevyo, matokeo take wanajikuta wakikata tamaa ya maisha pale wanapohitimu na kukaa muda mrefu mtaani bila kupata ajira,"alisema
Aidha katika wakati mwingine,Waziri amelielekeza Baraza la Elimu na Mafunzo ya Ufundi (NACTE), kuandaa mashindano hayo kila mwaka na kuhakikisha wanatanua wigo wa taasisi nyingi zaidi kushiriki katika mashindano hayo kutokana umuhimu wa mashindano hayo ikizingatiwa nchi inatekeleza kauli mbiu ya Tanzania ya viwanda.
"Naamini kupitia mashindano hayo mmepata fuksa ya kubadilishana mawazo, kujadili mbinu mbalimbali za kutatatua changamoto inayokabili sekta ya viwanda na Mafunzo ya ufundi kwa ujumla na kudumisha ushirikiano wa wadau katika eneo hilo," alisema.
Akizungumzia udahili, aliwasisitiza na kuwaasa wahitimu kupitia ngazi mbalimbali kutumia fulsa ya kufunguliwa kwa dirisha la udahili kuomba na kuahiliwa ili kwa maelekezo yaliyotolewa na Nacte waweze kujiunga na vyuo.
Kwa upande wake, Katibu Mtendaji wa Nacte, Adolf Rutayuga, alisema, maonesho hayo yatafanyika kila mwaka na Baraza litaendelea kuyaboresha ili yawe na tija zaidi na kuondoa mapungufu yaliyiojitakeza kwa mwaka huu ili mwakani yasijirudie.
Rutayuga alifafanua kuwa, anaamini mwaka maonesho hayo yatashirikisha taasisi nyingi zaidi ambazo kwa mwaka huu hazikupata fulsa ya kushiriki.
No comments:
Post a Comment