Bado siku 22 kabla ya michuano ya mataifa ya Afrika AFCON kuanza kutimua vumbi nchini Misri, ambapo timu takribani 24 zitashiriki.
Timu mbalimbali washiriki zimeshatangaza vikosi vyao vya awali, zingine zikitangaza vikosi vyao vya mwisho na zingine zikiwa tayari zipo kambini kujiwinda na michuano hiyo.
Leo tunaangazia kundi C ambalo linahusisha timu ya taifa ya Tanzania, 'Taifa Stars', Senegal, Algeria na Kenya, ambapo tunaangazia vikosi vya wapinzani wa Taifa Stars na namna nyota wao bora watakavyoweza kuleta ushindani mkali katika finali hizo.
Kikosi cha Kenya ambacho kimeondoka wiki hii kuelekea kambini nchini Ufaransa ni: Walinda lango, Patrick Matasi, John Oyemba, Faruk Shikalo: Mabeki, Abud Omar, Joash Onyango, Joseph Okumu, Musa Mohammed, David Owino, Bernard Ochieng, Brian Mandela, Philemon Otieno, Eric Ouma: Viungo, Victor Wanyama, Anthony Akumu, Ismael Gonzalez, Ayub Timbe, Francis Kahata, Ovella Ochieng, Dennis Odhiambo, Eric Johanna, Paul Were, Cliffton Miheso, Johanna Omollo: Washambuliaji, John Avire, Masud Juma, Christopher Mbamba, Michael Olunga.
Kocha wa timu ya taifa ya Algeria, Djamel Belmadi naye ametaja kikosi chake cha wachezaji 23 kuelekea katika michuano hiyo, ambapo Walinda lango, Rais M'bohli, Azzedine Doukha, Alexandre Oukidja: Mabeki, Aissa Mandi, Mehdi Zeffane, Ramy Bensebaini, Rafik Halliche, Mehdi Tahrat, Djamel Benramri, Youcef Atal, Mohamed Fares: Viungo, Haris Belkebla, Ismael Bennacer, Mehdi Abeid, Soufiane Feghouli, Adiene Guedioura, Hichem Boudaoui: Washambuliaji, Adam Ounas, Ryad Mahrez, Islam Slimani, Yacine Brahimi, Boughdad Bounedjah, Youcef Belaili.
Kocha wa Senegal, Aliou Cisse pia ametangaza kikosi chake cha wachezaji 25 ambao wataiwakilisha nchi hiyo katika michuano ya AFCON, ambapo Walinda lango ni, Edouard Mendy, Alfred Gomis, Abdoulaye Diallo: Mabeki, Kalidou Koulibaly, Salif Sane, Pepe Abou Cisse, Youssouf Sabaly, Moussa Wague, Lamine Gassama, Saliou Ciss: Viungo, Gana Gueye, Alfred Ndiaye, Badou Ndiaye, Sada Thioub, Krepin Diatta, Chekhou Kouyate, Sidy Sarr, Henri Samet: Washambuliaji, Santy Ngom, Moussa Konate, Mbaye Niang, Sadio Mane, Keita Balde, Ismaila Sarr.
Kundi hili lina wachezaji wachezaji wawili wanaotarajia kuchuana katika fainali ya Klabu Bingwa Ulaya kesho Jumamosi nchini Hispania, ambao ni Sadio Mane anayeichezea Liverpool na Victor Wanyama anayekipiga na Tottenham Hotspurs.
No comments:
Post a Comment