Simba inamuwania mshambuliaji wa Kagera Sugar Ramadhani Kapera aliyen'gara kwenye kikosi cha timu hiyo msimu huu
Wakati Simba ikitarajiwa kuwatoa kwa mkopo baadhi ya nyota wake ambao hawakuwa na mchango mkubwa, Kapera anatajwa kupendekezwa kuchukua nafasi ya Adam Salamba ambaye ni miongoni mwa watakaotolewa kwa mkopo
Mbali na Kapera, kiungo mshambuliaji wa Mtibwa Sugar Salum Kihimbwa ni miongoni mwa wachezaji wa ndani waliopendekezwa kusajiliwa na Simba
Mmoja wa viongozi wa Simba amethibisha kuwa tayari wameshajadiliana kusuhu usajili wa wachezaji hao pamoja na kiungo wa Gor Mahia Francis Kahata ambaye anasubiri kutua Msimbazi akiwa tayari ameaga kunako klabu yake ya Gor Mahia
Jana Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Mohammed Dewji alisema michakato ya usajili utaanza wiki ijayo na aliwatoa hofu mashabiki wa timu hiyo kuwa wachezaji wote waliopendekezwa na Aussems watasajiliwa kwa gharama yoyote
No comments:
Post a Comment