We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Friday, May 31, 2019

Waislam watakiwa kushirikiana kiimani katika shughuli za maendeleo


Na Rahel Nyabali,Tabora 

Waislam mkoani Tabora wametakiwa kuondoa tofauti zao kwa kushirikiana katika kumcha Mwenyezi Mungu  kuwa wa moja kiimani na katika shughuli za kimaendeleo ya kijamii ili kuimarisha umoja miongoni mwao bila kubaguana katika misikiti ya ibada. 

Wito huo umetolewa na Sheikh wa Mkoa wa Tabora Alhaj Ibrahim Mavumbi  wakati akiongea na Masheikh wa wilaya wa mkoa wa Tabora ofisini kwake amewataka masheikh kuandaa vijana wakiislamu kwa ajili ya mashindano ya kuhifadhi judhuu ambayo yatahudhuriwa na waumini wa dini mbalimbali juni 13 mwaka huu mjini Tabora. 

Katika kikao hicho Sheikh Mavumbi amewaomba waumini wa dini ya kiislam kuendelea na funga yao ya mwezi mtukufu wa ramadhani kwa kufuata misingi yote ya dini bila kusahau kumcha Mwenyezi Mungu. 

Aidha Wakiongea kwa niaba ya Masheikh wenzao Sheikh wa wilaya ya Nzega Mrisho Zahor na  Zaimu Ramadhan  kaimu Sheikh wa Urambo  wameahidi kusimamia maelekezo hayo kwa kuwaelimisha waumini wao, na kuhakikisha  umoja na ushirikiano  katika jamii.

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list