Mwimbaji wa RnB R.Kelly amefunguliwa mashtaka mengine 11 ya unyanyasaji wa kingono ikiwemo ya mmoja wa Wanawake anayemtuhumu kumyanyasa kingono akiwa chini ya miaka 18 inaelezwa kama akipatikana na hatia R.Kelly anaweza kufungwa mpaka miaka 30 jela.
Kwa mujibu wa mtandao wa ‘The Blast”umeripoti kuwa mwimbaji huyo alifunguliwa mashtaka hayo siku ya Alhamis May 30,2019huku Mwanasheria wa R.Kelly aliandika kupitia ukurasa wake wa twitter kuwa mwimbaji huyo hajafunguliwa kesi mpya bali ameshtakiwa na kosa ambalo lilikuwepo tokea zamani kwa hiyo shtaka hilo halibadilishi kitu.
Inaelezwa kuwa R .Kelly atatakiwa kurudi Mahakamani June 6 mwaka huu kwa ajili ya kusikiliza kesi yake mpya. Mwanzoni mwa mwaka huu msanii huyo alikabiliwa na mashtaka 10 ya unyanyasaji wa kingono hata hivyo alikana kuhusuka na vitendo hivyo na aliaachiwa huru kwa dhamana.
No comments:
Post a Comment