We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Monday, October 14, 2019

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi.

Leo tumekuletea habari njema ni kuwa tayari App mpya ipo playstore na unaweza kuidownload hapa chini ili kuendelea kupata habari zetu.

BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD APP YETU MPYA UKISHA BOFYA BONYEZA NENO OPEN IN PLAYSTORE KISHA INSTALL APP YETU MPYA!! NI RAHISI TU

Wednesday, October 2, 2019

Duniani Leo October 2, 2019 ( Sauti ya America VOA )

Bonyeza play hapa chini kutazama zaidi pia tembelea app hii kila Mara kusoma Habari Mpya

Mbunge CCM awajibu wanaosema hali ni ngumu

Mbunge wa Jimbo la Kinondoni,Abdallah Mtolea, amewatia moyo wale wote wanaolalamika kuhusu hali ngumu, kwakuwa ugumu wa maisha ndiyo kipimo cha maendeleo kwa mtu na kwamba hakuna nchi yoyote ambayo ilishawahi kuendelea bila kupitia nyakati ngumu

Mbunge Mtolea ametoa kauli hiyo, wakati akizungumza kwenye kipindi cha East Africa BreakFast cha East Africa Radio, ambapo amekiri kuwa hali ni ngumu na kuwataka wananchi wawe wavumilivu.
"Wengi wanasema hali ni ngumu ila niwaambie, hakuna nchi ambayo iliendelea kwenye hali ambayo ni nyepesi, lazima tupate maendeleo kwenye hali ngumu." amesema Mtolea.
Aidha akizungumzia suala la kuhama chama, Mtolea amesema kuwa hana mpango huo na ataendelea kuwa ndani ya Chama Cha Mapinduzi.
''2020 nitaendelea kuwa Chama Cha Mapinduzi, uzuri ukiwa CCM ukienda kwa kiongozi wa Serikali unakuwa kama umeenda kwa Baba, yaani ndiyo maana kila kitu kinaenda kiurahisi'' amesema Mtolea.

"Tunarudi kileleni tunakostahili" - Nugaz

Kuelekea mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara (VPL) kati ya Yanga na Polisi Tanzania, Msemaji na Afisa Muhamasishaji wa klabu hiyo, Antonio Nugaz amesema kuwa sasa wamerejea rasmi katika ligi na watatembeza kichapo kwa yeyote atakayetokea.

Akizungumza na EATV&EA Radio Digital katika Makao Makuu ya Klabu hiyo, Nugaz amesema kuwa kesho Alhamisi, mashabiki wa Yanga wantakiwa kuja kufurahi uwanjani kwakuwa kazi waliyonayo hivi sasa ni kukusanya kila pointi tatu zilizo mbele yao.
"Polisi Tanzania tulishawahi kucheza nao mechi ya kirafiki na tukapoteza dhidi yao, lakini wajue kabisa unapokuwa na Yanga mashindanoni ni tofauti kabisa unapocheza nayo kirafiki, hilo walizingatie", amesema Nugaz.
"Tunataka mashabiki wetu wafike uwanjani kusapoti timu yao, kesho tumejipanga kupambana kuhakikisha kila anayeshuka Dar es Salaam na hata nje ya Dar es Salaam tunachukua pointi tatu kuhakikisha tunarudi kileleni ambako Yanga inastahili kukaa", ameongeza.
Yanga ilipoteza mchezo wa kwanza wa ligi dhidi ya Ruvu Shooting kwa bao 1-0 na sasa iko katika nafasi za mwisho za ligi, ikiwa imecheza mchezo mmoja pekee.

Yaelezwa Pundamilia wa ajabu, aliyepatikana Kenya amehamia Tanzania, Fahamu zaidi

Pundamilia wa ajabu ambaye hivi karibuni alionekana katika mbuga ya wanyama ya Mara nchini Kenya amevuka mpaka na kuingia ndani ya Mbuga ya Wanyama ya Taifa ya Serengeti pamoja na pundamilia wengine waliokuwa wanahama pamoja na Nyumbu , limeripoti gazeti la Nation nchini Kenya
Kinyume na pundamilia wengine wenye mistari kwenye ngozi yake pundamilia huyo anamadoadoa meupe na mistari michache myeupe inayofifia mwilini mwake, jambo lililomfanya kuwa ni wa kipekee.
Taarifa ya kuhamia kwake nchini Tanzania imethibitishwa na makumi ya watalii na walinzi wa mbuga za wanyama pamoja na katibu wa shirika la madereva wa magari ya utalii nchini Kenya Felix Migoya ambaye amesema kuwa punzamilia huyo mchanga mwenye umri wa mwezi mmoja hivi , kwa sasa yuko katika eneo la kaskazini mwa mbuga ya wanyama ya Serengeti Serengeti.
Alipinga taarifa za uvumi kwamba kivutio hicho kipya cha utalii katika mbuga ya wanyama ya Mara kilikamatwa na kufungiwa kuhifadhiwa mahali pake kama ilivyoelezwa katika mitandao ya habari ya kijamii katika kipindi cha wiki tatu zilizopota, Limeripoti gazeti la Daily Nation nchini humo.
“Taarifa za mitandao ya kijamii ni feki , pundamilia anayeonyeshwa kwenye mitandao ya kijamii ni mkubwa na alikamatwa nchini Afrika Kusini katika tarehe ambayo haijulikani mika kadhaa iliyopita ,”alisema Bwana Migoya alipozungumza na gazeti la the Nation Jumatano.
Wazazi wa pundamilia huyo mchanga wako katika kipindi cha mwaka cha kuhama kwa zaidi ya mamilioni ya wildebeest baina ya mbuga ya wanyama ya Serengeti na hifadhi ya wanyama ya Maasai Mara – tukio ambalo huwavutia watalii kutoka maeneo mbali mbali duniani.

PundamiliaHaki miliki ya pichaNATION MEDIA GROUP

Tukio hilo, ambalo liliwekwa katika orodha ya ”Maajabu Saba ya Dunia ‘, kwa kawaida kuanza katikati ya mwezi Juni hadi mwezi Oktoba.
Katika kipindi hiki, nyumbu hukutana kabla ya kufanya safari yao ya kurejea sambamba na mamia ya pundamilia , swala na wanyama wengine wanaotafuta malisho.
Pundamilia huyu wa ajabu mweusi kwa mara ya kwanza aligunduliwa na kupigwa picha mapema mwezi Septemba karibu na mto Mara River na Antony Tira, mwongozaji maarufu wa safari za watalii kutoka kabila la Maasai na alimpiga picha hiyo katika kambi ya utalii ya Matira Bush iliyopo ndani ya mbuga ya wanyama.
Bwana Tira alimuita pundamilia huyo mchanga jina la baba yake ‘Tira’.
Si mweusi kabisa , na kutokana na utofauti wa ngozi yake katika sehemu mbali mbali za mwili wake: “Kutokana na rangi yake , pundamilia huyo amekuwa maarufu ghafla na amekuwa kivutio cha watalii katika mbuga ya Mara na sasa huenda watalii wakaelekea Serengeti kwani watu wengi wanamfuata kiumbe huyo wa ajabu ,” aliongeza Bwana Migoya.
Tangu mpigapicha Tira alipotuma picha ya pundamilia huyo na kuwaalika watu kuja kumuona, watu wengi wamekuwa wakiongezeka katika hifadhi ya wanyama ya Mara na kusababisha ‘msongamano ‘ mkubwa wa watukatika hifadhi hiyo..

RUKWA: Wapigwa na radi wakinywa pombe kilabuni, Wanne wafariki dunia papo hapo

Watu wanne wamekufa papo hapo na wengine 7 kujeruhiwa baada ya kupigwa na radi wakiwa kilabuni wakinywa pombe katika kitongoji cha Nkata kijiji cha Kate, Nkasi mkoani Rukwa.
Akizungumzia tukio hilo, Mwenyekiti wa Kijiji cha Kate, Amesema kuwa watu hao walikuwa wanakunywa pombe katika kilabu hicho, ghafla ilipiga radi katika eneo hilo,  hali iliyosababisha watu wengi kuanguka na kupoteza fahamu.
Baada ya kuwafanyia uchunguzi watu hao waliokuwa katika kilabu hicho, Mwenyekiti amesema  ilibainika wanne kati yao wamefariki dunia papo hapo na wengine kujeruhiwa na kupelekwa kwenye zahanati ya Kanisa Katoliki iliyoko kijijini hapo. Ambapo baada ya kufikisha hapo kwa huduma, wengine walizinduka na kuruhusiwa kurudi nyumbani.
Mwenyekiti huyo aliwataja waliofariki dunia kuwa ni John Sumuni (31), Akleo Feluzi (45), Boniface Fundililwa (38) na Anastazia Njali (48) wote wakazi wa kijiji hicho.
Naye, Mganga Mfawidhi wa zahanati ya Kate Mission, Elly Joseph, alikiri kuwapokea majeruhi zaidi ya 10 na baada ya kuwapatia huduma ya kwanza, wengi wao waliruhusiwa kurudi nyumbani na wanne waliokuwa  mahututi walibaki na wanaendelea na matibabu.
Tayari Mkuu wa Wilaya ya Nkasi, Said Mtanda, amekiri kutokea kwa tukio hilo na kuthibitisha kuwa watu wanne ndio waliopoteza maisha na kuwa wako kwenye kikao baada ya hapo yeye na viongozi wenzake watakwenda katika kijiji hicho kuwajulia hali majeruhi na kushiriki mazishi ya watu waliopoteza maisha.
Chanzo: Nipashe

Mahakama Kuu Kanda Ya Dar Es Salaam Kusikiliza Kesi 3,372

Na Aziza Muhali- (SJMC)
Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, inaendelea kusikiliza kesi 3,372 zilizosajiliwa Mahakamani hapo kwa sasa, zikiwamo za madai, jinai na ardhi.

Hayo yamesemwa na Naibu Msajili Mfawidhi, Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Mhe. Joachim Tiganga, wakati akitoa elimu kwa umma kuhusu utoaji wa huduma  zinazotolewa  na mahakama hiyo, uliofanyika leo, Oktoba 2, mwaka huu katika ukumbi wa Mahakama Kuu, uliopo jijini Dar es Salaam.

Mhe. Tiganga  alisema  lengo la kutoa elimu hiyo  kwa wananchi ni kueleza huduma zinazotolewa na mahakama hiyo pia kupokea maoni na mapendekezo kutoka kwa wateja wao.

Akifafanua kuhusu kesi hizo, alisema kesi zinazoripotiwa kwa wingi ni kesi za madai ya kawaida ambazo ni 2,169 zikifuatiwa na kesi za jinai 789, wakati kesi za ardhi ni 354.

“Hivyo kutokana na idadi hiyo ya kesi, jaji mmoja anasikiliza kesi zipatazo 450 kwa mwaka badala ya kesi 220 kutokana na kuwepo kwa idadi ndogo ya majaji” alisema.

Aliongeza kuwa Mahakama hiyo ina jumla ya majaji saba, wakati idadi kamili inayohitajika ni 15, hivyo ina upungufu wa majaji 8.

Akizungumzia kuhusu ukataji rufaa, ambapo baadhi ya wananchi walitaka kufahamu juu ya utaratibu wake,ambao ni Farida Mwalwaka mkazi wa Toangoma na Ally Idd mkazi  wa Majimatitu, jijini Dar es Salaam, alisema kwamba mahakama  huwawezesha wateja wake kukata rufaa kwa kuwapatia nakala za kumbukumbu zote za kesi.

Aidha  Tiganga  aliwataka wananchi wenye malalamiko kuhusu uendeshwaji wa kesi mbalimbali  kufika katika dawati la malalamiko ambalo hufanyika siku ya Jumanne na Alhamisi kila wiki.

Kwa upande wake Hakimu Mhe. Joyce Karata, amewataka wananchi kuwa makini wakati wa utaratibu wa ukataji wa rufaa ambapo amesema kuwa rufaa inatakiwa kukatwa ndani ya muda, ili kuondoa usumbufu wa upatikanaji wa nyaraka.

LIVE: TAZAMA TAARIFA YA HABARI YA AZAM TV

Bonyeza play hapa chini kutazama zaidi pia tembelea app hii kila Mara kusoma Habari Mpya

LIVE: TAZAMA TAARIFA YA HABARI YA TBC ONE

Bonyeza play hapa chini kutazama zaidi pia tembelea app hii kila Mara kusoma Habari Mpya

LIVE: TAZAMA TAARIFA YA HABARI YA ITV

Bonyeza play hapa chini kutazama zaidi pia tembelea app hii kila Mara kusoma Habari Mpya

LIVE: ITAZAME MECHI YA GENK VS NAPOL

Link: 1

BONYEZA HAPA KUITAZAMA MECHI HII LIVE KUMBUKA KUBONYEZA X HAPO JUU KAMA UNAVYOONA KWENYE PICHA ENDAPO UTAONA MATANGAZO

MAKONDA KUBANANISHWA MBELE YA DR. BASHIRU, MAMA SAMIA "ATUELEZE AMEFANYA NINI? "

Bonyeza play hapa chini kutazama zaidi pia tembelea app hii kila Mara kusoma Habari Mpya

Wambura aomba msamaha na kukiri makosa yake kwa DPP

Aliyekuwa Makamu wa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania(TFF), Michael Wambura ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi kisutu kuwa ameandika barua kwa Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini(DPP) kwa ajili ya kuomba msamaha na kukiri makosa yake.
Wambura alifikishwa Mahakamani hapo kwa mara ya kwanza Februari 11 mwaka huu akikabiliwa na mashtaka 17 yakiwemo ya kutakatisha fedha zaidi ya Tsh.Mil 100, katika kesi ya uhujumu uchumi namba 10/2019.
Hayo yamebainika mbele ya Hakimu Mfawidhi, Kelvin Mhina baada ya Wambura kueleza kuwa ameandika barua kwa DPP ili kuomba msamaha na kukiri makosa yake hivyo anauomba upande wa mashtaka kufuatilia ili aweze kupata haki yake.
Baada ya maelezo hayo Hakimu Mhina ameahirisha shauri hilo hadi Oktoba 16, 2019 itakapokuja kwa ajili ya kutajwa.
MBEYA BOY “NILIKOPA NIKATE

ACT-Wazalendo wajipanga kupinga uteuzi wa mkurugenzi NEC mahakamani - VIDEO



Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe amesema chama hicho kimemuagiza wakili, Jebra Kambole kuangalia misingi ya kisheria ili kufungua kesi ya kupinga uteuzi wa mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Dk Wilson Charles.

Ametoa kauli hiyo leo Jumatano Septemba 2, 2019 muda mfupi baada ya kutoka kusikiliza kesi ya kupinga ukomo wa urais iliyofunguliwa na Dezydelius Mgoya ambayo chama hicho kimeomba kujumuishwa.
Akiwa katika viwanja vya Mahakama Kuu, Dar es Salaam Zitto amesema wameshangazwa na uamuzi wa Rais John Magufuli kumteua Charles aliyewahi kugombea ujumbe wa halmashauri kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (NEC).
“Suala hili la wasimamizi wa uchaguzi ambao ni wanachama wa vyama vya siasa kuteuliwa lipo mahakamani, kuna kesi imefunguliwa na Bob Wangwe na wanasheria pamoja na wanaharakati.”
“Mahakama ikatoa amri kwamba  wasimamizi wa uchaguzi hawapaswi kuwa wanachama, makada au mashabiki  wa vyama vya siasa,” amesema Zitto.


Amesema kitendo cha kuteuliwa kwa Wilson ni dharau kwa mahakama ambayo imeshatoa uamuzi kuwa hawapaswi kusimamia uchaguzi.
Amebainisha kuwa kulingana na suala hilo kuwa muhimu, wanashauriana na vyama vingine vya siasa kwa ajili ya kuchukua hatua za kisheria kuzuia uteuzi huo.
“Tumeshamuagiza Kambole atazame misingi ya kisheria ili kuhakikisha tunazuia uteuzi. Tunahitaji uchaguzi huru tunaangalia namna bora ya kuweza kuchukua hatua za kisheria.”
“Tunataka wakili atazame jambo hili kulingana na uamuzi wa mahakama katika kesi ya awali (ambayo Serikali ilikata rufaa) na sasa tunasubiri uamuzi wa rufani ili kuhakikisha tunazuia uteuzi wa wanasiasa kusimamia uchaguzi,” amesema Zitto.

TAKUKURU inachunguza mradi wa BILIONI 12 machinjio ya Vingunguti DSM (+video)

Leo October 2, 2019 Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (TAKUKURU) imesema inafuatilia kwa ukaribu mradi wa ujenzi wa machinjio ya Vingunguti na soko la Kisutu.
Tutakamilisha ufatiliaji wa mradi wa ujenzi wa machinjio ya Vingunguti wenye thamani ya Tsh. Billion 12, kama mnavyofahamu mradi ule unafuatiliwa sana na sisi kama TAKUKURU tunaufatilia ili kuhakikisha hakuna uvujaji wa pesa za umma, pia tutaendelea kufanya ukaguzi soko la Kisutu” – Kamanda wa TAKUKURU Ilala, Christopher Myava.

Dwayne ‘The Rock’ Johnson amaliza bifu lake na Vin Diesel, Atangaza kurudi kwenye mieleka

Muigizaji wa filamu kutoka nchini Marekani, Dwanye Johnson maarufu kwa jina la The Rock, ametangaza rasmi kuwa ameweka kando tofauti zake na rafiki yake Vin Diesel.
The Rock kupitia ukurasa wake wa Instagram, Amewashukuru mashabiki zake ambao walikuwa wanataka bifu hilo limalizike ili waendelee na kazi zao kama ilivyokuwa awali kwenye filamu ya Fast & Furious.
Kwenye video hiyo, The Rock amesikika akisema, “Napenda kutumia nafasi hii kuwashukuru mashabiki wote ambao walikuwa wanataka tuweke pembeni tofauti zetu, kutoka kwa mashabiki jambo hilo limefanikiwa na sasa hakuna tofauti kati yetu, urafiki kama kawaida.
“Nakushukuru Vin Diesel kwa sapoti yako kwa kuifanya filamu ya Hobbs &  Show kufanya viizuri sokoni kwa muda mfupi imetengeneza dola milioni $750. Yeye ndiye aliyenifanya niwe maarufu kwenye familia ya Fast & Furious miaka 10 iliyopita ” amesema The Rock.
Kwa upande mwingine, The Rock ametangaza kurudi tena kwenye mieleka (WWE) ambapo amesema bado anajiona mwenye nguvu.
Awali, The Rock alitangaza kustaafu mchezo huo wa mieleka na kuahidi mashabiki wake kuwa atabaki kwenye uigizaji wa filamu tu.

Kulthum Mansooor wa Takukuru amwandikia DPP barua ya kukiri makosa

Leo October 2, 2019 Aliyekuwa Mkurugenzi wa Mipango, Ufuatiliaji na Tathimini wa TAKUKURU, Kulthum Mansoor amemuandikia barua Mkurugenzi wa Mashtaka nchini(DPP) kwa ajili ya kukiri makosa yake .
Mansoor anakabiliwa na mashtaka manane ya kughushi, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na kutakatisha Sh.Bil 1.477.
Hayo yamebainika baada ya Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon kumueleza Hakimu Mfawidhi, Kelvin Mhina wa kuwa bado upelelezi wa kesi haujakamilika.
Baada ya kueleza hayo, Wakili wa Utetezi, Elia Mwingira amedai kuwa wameandika barua kwenda kwa DPP kwa ajili ya kuomba msamaha na kukiri makosa hivyo ni vyema kupata majibu kwa haraka ili mshtakiwa aweze kupata haki yake ya msingi.
“Tunaomba upande wa mashtaka kulifuatilia hili ili mteja wetu aweze kupata haki yake ya msingi,” alidai Mwingira.
Baada ya maelezo hayo Wakili Simon amedai kuwa suala hilo atalifuatilia kwa haraka zaidi.
Hakimu Mhina ameahirisha shauri hilo hadi Oktoba16, 2019 itakapokuja kwa ajili ya kutajwa.

Naibu Waziri Kanyasu: Ujenzi Wa Bwawa La Kufua Umeme La Julius Nyerere Limezingatia Masuala Ya Usalama Wa Uhifadhi

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu amesema nia ya Serikali ya ujenzi wa bwawa  la kufua umeme la Julius Nyerere iko pale pale na ujenzi wake unaendelea kwa kasi huku ukizingatia masuala ya Uhifadhi katika Pori la Akiba la Selous.

Akizungumza leo na Wabunge wa Kamati ya Bunge ya Mazingira, Uhifadhi wa Maliasili na Usalama wa Nyuklia kutoka Ujerumani Mhe. Kanyasu  amesema Tathmini ya Athari kwa Mazingira imefanyika na kuonyesha kuwa ujenzi huo ni salama katika shughuli za Uhifadhi.

“Serikali ya Awamu ya Tano inatekeleza mradi huu kwa kutumia fedha zake kutoka vyanzo vya ndani. Mradi huu utachukua eneo la ukubwa wa kilomita za  mraba 1,250 ambalo ni sawa na asilimia tatu (3%) tu ya eneo lote la pori la akiba selous lenye ukubwa wa kilomita za mraba 50,000.” Mhe. Kanyasu alisisitiza.

Mhe. Kanyasu amesema  kiwango cha umeme cha megawati 2,100 kitakachozalishwa katika gridi ya Taifa itasaidia kwa kiasi kikubwa kuokoa misitu inayokatwa kwa kasi kwa ajili ya nishati ya mkaa na kuni.

Aidha, Mhe. Kanyasu amewaeleza Wabunge hao kuwa ujio wa Bwawa hilo la Umeme limepelekea sehemu ya Pori la Akiba la Selous kupandishwa hadhi na kuwa Hifadhi ya Tiafa ya Julius Nyerere ambapo kufuatia hali hiyo ulinzi wa wanyamapori katika Hifadhi hiyo utakuwa madhubuti zaidi na ilivyokuwa mwanzo.

Katika hatua nyingine Mhe. Kanyasu amewaeleza Wabunge hao kuwa Serikali ya Tanzania imelichukua suala la mabadiliko ya tabia ya nchi kwa uzito unaostahili na kwa kutambua athari zake kwa mwaka huu imepandisha hadhi mapori ya akiba manne na  kuwa Hifadhi za Taifa na hivyo ulinzi wake wa Hifadhi hizo umeongezeka maradufu

Kwa upande wake Kiongozi wa ujumbe huo Mhe. Sylvia Kotting- Uhl ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa mageuzi makubwa yanayofanyika katika kipindi cha Serikali ya Awamu ya Tano katika masuala ya Uhifadhi  na kuahidi ushirikiano na nchi yake katika kujenga uwezo katika nyanja za kusimamia na kudhibiti taka za kielektroniki, Uzalishaji wa Umeme wa jua na kutoa mwaliko kwa ujumbe wa Tanzania kutembelea Ujerumani

Aidha, Mhe.Sylvia amesema licha ya ujenzi wa Bwawa la Umeme la Julius Nyerere bado wataendelea kuisaidia Serikali ya Tanzania katika masuala ya Uhifadhi kufuatia juhudi kubwa za Serikali ya awamu ya tano ya kuendelea kutunza na kuhifadhi maeneo yasiweze kuharibiwa na shughuli za kibinadamu.

Maabara Bubu 13 Zafungiwa, Huku 48 Zikipewa Onyo Kali

Na Rayson Mwaisemba WAMJW- DODOMA
SERIKALI kupitia Wizara ya Afya, imezifungia jumla ya maabara 13, ambazo ni sawa na asilimia 21% kati ya Maabara 61 zilizokaguliwa, huku ikitoa onyo kali kwa Maabara 48 kutokana na baadhi ya Maabara hizo kutokidhi viwango vya kutoa huduma za upimaji.

Hayo yamesemwa leo na Msajili wa Bodi ya Maabara Binafsi kutoka Wizara ya Afya Bw. Dominic John Fwiling’afu wakati wa ziara ya ukaguzi wa hali ya utoaji huduma za upimaji katika maabara zilizopo Jiji la Dodoma.

“Tuliweza kufunga Maabara 13, kati ya maabara 61 tulizozikagua, na hizo maabara 13 ni sawa na asilimia 21% ambazo tuliweza kuzifungia, huku Maabara 8 sawa na asilimia 20% ni Maabara zilizo ndani ya vituo vya kutolea huduma kama vile zahanati, na maabara zinazojitegemea ni 5 sawa na asilimia 24%” amesema Bw. Dominic Fwiling’afu

Amesema kuwa Bodi ya Maabara Binafsi katika kutekeleza majukumu yake, inaendeleza mpango wake wa kukagua Maabara Binafsi zote nchini ili kuhakikisha zinatoa huduma kulingana na miongozo ili kutoa huduma bora kwa Wananchi.

Aliendelea kusema kuwa zoezi hilo limeanza Jijini Dodoma, huku lengo likiwa kukagua jumla ya Maabara 106 ili kujiridhisha utoaji huduma sahihi kwa wananchi, ikiwemo kukagua kama Wataalamu waliopo wanakidhi vigezo kwa mujibu wa Sheria.

Pia, Bw. Dominic Fwiling’afu amesema kuwa licha ya kukagua ili kujiridhisha na ubora wa huduma zinazotolewa na Maabara hizo, Bodi hiyo inajukumu la kuangalia ulipaji wa tozo mbali mbali uliowekwa kwa mujibu wa Sheria na kujiridhisha kama Maabara hizo zimetimiza masharti wakati wa uanzishwaji wake.

“Sambamba na hiyo Bodi ya Maabara Binafsi inajukumu la kuangalia ulipwaji wa tozo mbali mbali katika uendeshwaji wa Maabara hizo, kama zote zinafuata miongozo kwa mujibu wa Sheria na kuangalia utendaji na utoaji huduma katika Maabara hizo kama ni salama na sahihi” amesema Bw. Dominic Fwiling’afu

Aidha, Bw. Dominic Fwiling’afu ameongeza kuwa, mbali na kuzifungia baadhi ya Maabara hizo ambazo hazijakidhi vigezo kulingana na Sheria na miongozo, Bodi imeendelea kutoa ushauri kwa wamiliki na Wataalamu wa Maabara ili kutoa huduma bora kwa Wananchi.

Mbali na hayo, Bw. Dominic Fwiling’afu ametoa wito kwa wananchi kuhakikisha wanapata huduma kwenye Maabara zilizosajiliwa na kutambulika kwa mujibu wa Sheria, huku akiwaagiza Wamiliki wa Maabara binafsi kuhakikisha wanabandika leseni ya usajili wa Maabara hizo katika eneo la mapokezi ili kiweze kuonekana.

Akielezea sababu za kuzifungia baadhi ya Maabara, Mkaguzi kutoka Bodi ya Maabara Binafsi Wizara ya Afya Bi. Mayasa Rico amesema kuwa kukosekana kwa Wataalamu wa Maabara wenye sifa, kuendesha Maabara hizo bila ya kuwa na vibali, kutokuwa na miongozo na kanuni ya Bodi, miundombinu kutokidhi viwango, kutoa huduma za matibabu na kutoa huduma baadhi ya huduma bila kibali.

“Kukosekana kwa Wataalamu wenye sifa, kuendesha Maabara bila kuwa na vibali,kutokuwa na miongozo na kanuni ya Bodi,majengo kutokidhi viwango kulingana na taratibu, kupima vipimo visivyoruhusiwa bila ya vibali na kutoa huduma za matibabu ndani ya Maabara ni baadhi ya sababu zinazopelekea kufungwa kwa Maabara hizo” amesema Bi. Mayasa.

Kwa upande wake, Mkaguzi kutoka Bodi ya Maabara Binafsi Wizara ya Afya Edinanth Ģareba, amedai kuwa jumla ya maabara 42 tu ndio zimesajiliwa na kutambulika kisheria kati ya Maabara 61 zilizo kaguliwa, ambazo ni sawa na asilimia 69%, huku akisisitiza kusajili Maabara hizo jambo litalosaidia kuzifuatilia Maabara hizo kwa ukaribu na kuzisa idia namna bora ya kutoa huduma ya vipimo kwa wananchi.

Aidha, Edinanth Ģareba aliendelea kutoa onyo kali kwa wauguzi na tabibu wanaopima sampuli za wagonjwa, na kusisitiza kuwa shughuli zote za maabara zinapaswa kufanywa na Mtaalamu wa Maabara tu na si vinginevyo.

CEO Mpya Simba ashangazwa na Simba kusajili wachezaji kutoka Brazil

CEO wa Simba Senzo Mazingiza amekuja na mkakati ambao utaiwezesha klabu hiyo kupunguza matumizi yasiyo ya lazima
Senzo aliyeingia ofisini mwezi uliopita akichukua nafasi ya Crescentius Magori ambaye mkataba wake ulimalizika, ameweka mkakati huo baada ya kutoridhishwa gharama ambazo Simba imekuwa ikitumia
Moja ya mambo ambayo ameyafanyia kazi kwa haraka, ni kukamilika kwa ujenzi wa uwanja wa Simba ulioko Bunju jijini Dar es salaam
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Mohammed Dewji tayari ameahidi Simba huenda ikaanza kufanya mazoezi kwenye uwanja huo kuanzia mwishoni mwa mwezi huu
Simba imekuwa ikitumia uwanja wa Gymkhana kwa ajili ya mazoezi ambao gharama yake kwa siku ni Tsh 500,000/-. Wakati mwingine hutumia uwanja wa Boko Veterans ambao gharama yake sio chini ya 300,000/-
Pia inaelezwa Senzo amehamisha kambi ya Simba iliyokuwa ikiwekwa Sea Scape Hotel
Bosi huyo ameahidi kufuatilia kwa ukaribu michakato ya usajili iliyofanyika
Ameeleza kushangazwa na Simba kusajili wachezaji kutoka Brazil

Wazee CHADEMA Wavunja Ukimya

Baraza la Wazee la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), limeitaka serikali kurejea ahadi yake ya kumalizia mchakato wa katiba mpya iliyoitoa mwaka 2015 wakati wa uchaguzi mkuu.
Wazee hao wamedai kuwa  mchakato huo bado una umuhimu mkubwa kwa Watanzania.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Baraza hilo, Hashim Juma Issa, alidai kushangazwa na ukimya wa serikali kuhusu mchakato huo ambao uligharimu fedha nyingi za Watanzania.

Wazee hao wanadai kusitishwa kwa mchakato huo ni hasara kubwa kwa Taifa kwa kuwa mchakato huo ulishaanza na umegharimu fedha nyingi, hivyo kutaka uendelezwe kwa maslahi ya Taifa.

Katika hatua nyingine, wazee hao wamelalamikia kuingiliwa kwa mikutano ya wabunge wa chama hicho na Jeshi la Polisi, wakidai kitendo hiko ni ukiukwaji wa misingi ya demokrasia nchini na kounya kuwa vitendo hivyo vinaweza kupelekea uvunjifu wa amani.

Kuhusu uchaguzi wa serikali za mitaa,  wameapa kulinda kura kwa madai ya kuchoka kuibiwa kura kila uchaguzi unapofika, na kulionya Jeshi la Polisi kuwa waangalifu katika uchaguzi huo ili kuepusha uvunjifu wa amani.

Mwandishi wa Habari Erick Kabendera Amuomba Rais Magufuli Amsamehe

Siku moja baada ya Rais John Magufuli kuongeza siku saba kwa washtakiwa wa makosa ya uhujumu uchumi, ambao hawajawasilisha maombi yao, Mwandishi wa Habari Erick Kabendera, anayekabiliwa na kesi hiyo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, amejitokeza kuomba radhi.

Ombi hilo lilitolewa jana na Wakili Jebra Kambole kwa niaba ya Kabendera, baada ya mwandishi huyo kupandishwa tena kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kufuatia makosa matatu yanayomkabili.

Mwandishi wa habari huyo alipandishwa kizimbani kwa madai ya kuongoza kundi la uhalifu kwa lengo la kupata faida au manufaa mengine, kutokulipa kodi kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ya zaidi ya Sh. milioni 173.2 na utakatishaji wa fedha kiasi cha zaidi ya Sh. milioni 173.24.

Wakili Jebra alidai Kabendera amemwomba radhi Rais Magufuli akieleza kwamba kama katika utekelezaji wa majukumu yake ya uanahabari kuna eneo alifanya makosa au aliteleza, amsamehe ili awe huru.

Aidha, Wakili Jebra alisema Kabendera yuko tayari kufanya jambo lolote, ili kulinda uhuru na usalama wake.

Kabendera, mwandishi wa habari za uchunguzi ndani na nje ya nchi, alichukuliwa na Jeshi la Polisi nyumbani kwake Mbweni, jijini Dar es Salaam Julai 26, mwaka huu, kabla ya kufikishwa mahakamani.

Katika kesi ya msingi,  mshtakiwa anadaiwa katika siku tofauti kati ya Januari 2015 na Julai 2019 jijini Dar es Salaam, alitoa msaada katika genge la uhalifu kwa nia ya kujipatia faida.

Katika shtaka la pili, inadaiwa siku na mahali hapo mshtakiwa bila kuwa na sababu za msingi kisheria alishindwa kulipa kodi ya Sh173.24 milioni ambayo ilitakiwa ilipwe kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Katika shtaka la utakatishaji fedha,  kati ya Januari 2015 na Julai 2019 ndani ya jiji na mkoa wa Dar es Salaam mshtakiwa alijipatia kiasi hicho cha Sh173.2 milioni wakati akizipokea alijua kuwa fedha hizo ni mazao ya makosa tangulizi ya kukwepa kodi na kujihusisha na genge la uhalifu.

Kimbunga cha Arusha mmoja adaiwa kuzama Ziwani

Mtu mmoja amezama na mtumbwi katika Ziwa Momella, lililopo katika mbuga ya Arusha, baada ya mtumbwi aliokuwa nao kupigwa na dhoruba, iliyosababishwa na kimbunga kikubwa kilichozua taharuki kwa wakazi wa mkoa huo siku ya jana.

Akizungumza na EATV & EA Radio Digital, leo Oktoba 2, 2019, Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha ACP Koka Moita, amesema kuwa mtu huyo anadaiwa kuzama majira ya saa 9:00 jioni siku ya Oktoba 1, lakini licha ya jitihada za uokozi kufanyika  hawakuweza kumpata.
''Wilaya ya Arumeru katika mbuga ya Arusha ndani ya ziwa Momella, kulikuwa na watalii wawili waliokuwa wamekodisha mitumbwi, upepo ulivyokuja ulileta  dhoruba na mitumbwi ikaanza kuyumba, lakini mtumbwi mmoja uliweza kutoka salama lakini yule nahodha wa mtumbwi wa pili ambaye ni mtanzania alizama na siku ya jana hatukufanikiwa kumpata'', amesema Kamanda Moita.
Kamanda Moita ameongeza kuwa juhudi za kumuokoa mtu huyo zinaendelea kwa kushirikiana na Jeshi la polisi, TANAPA  pamoja na Jeshi la Zimamoto na uokoaji.
Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list