Aliyekuwa Makamu wa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania(TFF), Michael Wambura ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi kisutu kuwa ameandika barua kwa Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini(DPP) kwa ajili ya kuomba msamaha na kukiri makosa yake.
Wambura alifikishwa Mahakamani hapo kwa mara ya kwanza Februari 11 mwaka huu akikabiliwa na mashtaka 17 yakiwemo ya kutakatisha fedha zaidi ya Tsh.Mil 100, katika kesi ya uhujumu uchumi namba 10/2019.
Hayo yamebainika mbele ya Hakimu Mfawidhi, Kelvin Mhina baada ya Wambura kueleza kuwa ameandika barua kwa DPP ili kuomba msamaha na kukiri makosa yake hivyo anauomba upande wa mashtaka kufuatilia ili aweze kupata haki yake.
Baada ya maelezo hayo Hakimu Mhina ameahirisha shauri hilo hadi Oktoba 16, 2019 itakapokuja kwa ajili ya kutajwa.
MBEYA BOY “NILIKOPA NIKATE
No comments:
Post a Comment