Muigizaji wa filamu kutoka nchini Marekani, Dwanye Johnson maarufu kwa jina la The Rock, ametangaza rasmi kuwa ameweka kando tofauti zake na rafiki yake Vin Diesel.
The Rock kupitia ukurasa wake wa Instagram, Amewashukuru mashabiki zake ambao walikuwa wanataka bifu hilo limalizike ili waendelee na kazi zao kama ilivyokuwa awali kwenye filamu ya Fast & Furious.
Kwenye video hiyo, The Rock amesikika akisema, “Napenda kutumia nafasi hii kuwashukuru mashabiki wote ambao walikuwa wanataka tuweke pembeni tofauti zetu, kutoka kwa mashabiki jambo hilo limefanikiwa na sasa hakuna tofauti kati yetu, urafiki kama kawaida.
“Nakushukuru Vin Diesel kwa sapoti yako kwa kuifanya filamu ya Hobbs & Show kufanya viizuri sokoni kwa muda mfupi imetengeneza dola milioni $750. Yeye ndiye aliyenifanya niwe maarufu kwenye familia ya Fast & Furious miaka 10 iliyopita ” amesema The Rock.
Kwa upande mwingine, The Rock ametangaza kurudi tena kwenye mieleka (WWE) ambapo amesema bado anajiona mwenye nguvu.
Awali, The Rock alitangaza kustaafu mchezo huo wa mieleka na kuahidi mashabiki wake kuwa atabaki kwenye uigizaji wa filamu tu.
No comments:
Post a Comment