We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Friday, July 12, 2019

BREAKING: Barcelona yamng'oa Antoine Griezmann Atletico Madrid kwa euro milioni 120

Miamba ya soka Uhispania klabu ya Barcelona imemsajili msahmbuliaji wa Ufaransa Antoine Griezmann kutoka klabu pinzani ya Atletico Madrid kwa kitita cha euro milioni 120.
Mshambuliaji huyo mwenye miaka 28 alikuwa sehemu ya kikosi cha timu ya taifa ya Ufaransa kilichonyakua kombe la dunia mwaka jana.
Griezmann ameingia mkataba wa miaka mitano na Barcelona ambao umeweka sharti la euro milioni 800 kwa klabu yeyote itakayotaka kumng'oa Nou Camp.
Mshambuliaji huyo machachari alijiunga na Atletico akitokea Real Sociedad mwaka 2014 na ameifungia Atletico magoli 133 katika michezo 256.
Mwaka mmoja uliopita, Juni 2018, alisaini mkataba mpya na Atletico wa miaka mitano, hata hivyo ilipofika mwezi Mei mwaka huu akatangaza kuwa ataihama klabu hiyo katika dirisha la usajili la majira haya ya joto.
Griezmann sasa anakuwa mchezaji wa sita ghali zaidi duniani kusajiliwa nyuma ya Neymar, Kylian Mbappe, Philippe Coutinho, Joao Felix na Ousmane Dembele

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list