Kampuni ya GSM imepewa jukumu la kutengeneza na kusambaza jezi za Yanga baada ya kushinda zabuni iliyotangazwa kwa mara ya pili hivi karibuni
Moja ya masharti yaliyokuwa yametolewa kwa mzabuni, ni kujenga duka la kuuza jezi na vifaa mbalimbali vya Yanga Makao Mkuu ya klabu
Baada ya mchakato huo kukamilika, sasa ni rasmi kampuni ya GSM pamoja na majukumu mengine, itaweka duka la kuuza jezi Makao Makuu ya klabu ya Yanga
Hakuna shaka baada ya mchakato huo kukamilika, Wanayanga watakuwa na uhakika wa kununua jezi halisi za klabu yao
Akizungumza na Waandishi wa Habari mapema leo, Makamu Mwenyekiti wa Yanga Fredrick Mwakalebela aliwataka wanachama na mashabiki wa timu hiyo kuachana na kasumba ya kununua jezi zisizo rasmi.
"Mzabuni wa kutengeneza jezi za klabu wa Yanga amepatikana"
"Mchakato wa kwanza ulipata wazabuni sita tukavunja na kuanza upya kutokana na mapungufu ya hapa na pale tukaanza upya ambapo tulipata wazabuni watatu ambao ni Just fit, Vunja Bei na GSM," alisema
"Vigezo ambavyo tuliwapa ilikuwa ni pamoja na uwezo wa kutengeneza jezi kwa wingi zenye ubora,kujenga duka Makao Makuu kwa gharama zao na mshindi wa zabuni hiyo ni GSM
"GSM itahusika kuuza jezi zenye nembo ya Yanga kuanzia wiki ya wananchi"

No comments:
Post a Comment