Kikosi cha Yanga leo kimefanya mazoezi ya mwisho kwenye Uwanja wa Technical Football mjini Ndola, kisha kuhamia kwenye uwanja wa Levy Mwanawasa ambako mchezo dhidi ya Zesco United utapigwa hapo kesho Jumamosi
Maandalizi hayo yalisimamiwa kikamilifu na kocha Mwinyi Zahera aliyeonekana kuridhika na mwenendo wa timu yake tangu walipowasili nchini Zambia siku tatu zilizopita
Zahera amesema ana matumaini makubwa kwa vijana wake kuelekea mchezo huo
Ari ya mchezaji mmoja mmoja pamoja na timu kwa ujumla iko juu
Mchezo utapigwa saa tisa Alasiri kwa saa za Zambia ambayo ni saa kumi jioni Tanzania
No comments:
Post a Comment