Mwanamke huyo kwa jina , Annet Namata, alikuwa amekiri kosa hilo na akaomba msamaha kwa madai kuwa yeye ni mama wa watoto watatu , limeripoti gazeti hilo.
Hakimu katika mahakama ya Mukono anaripotiwa kusema kwua alipunguza hukumu hiyo kutoka kifungo cha miaka saba hadi miaka miwili kwasababu mwanamke huyo “aliisaidia mahakama kwa kutopoteza muda wake ” kwa kukiri kosa.
Taarifa ya hukumu dhidi ya Bi namata imeibua hisia kali miongoni mwa Waganda huku wengine wakijiuliza ni vipi aliamua kutekeleza kitendo hicho:
Tukio hilo lilitokea miezi mitatu iliyopita katika kijiji cha Kitega yapata kilomita 46 (maili 28 ) emashariki mwa mji mkuu wa Uganda Kampala.
Mume wake anaripotiwa kutofurahishwa na hukumu iliyotolewa na alitaka mkwe wake afungwe kwa muda mrefu zaidi.
Gazeti la Uganda Observer mwezi uliopita liliripoti kwamba mwanamke huyo alikabidhiwa kwa polisi na mume wake ambaye alifahamishwa tukio hilo la wanakijiji.
Inaripotiwa kuwa Bi Janet Namata alichanganya damu ya hedhi na chakula na baadae kumlisha binti yake wa kambo.
Vyombo vya habari pia vimeripoti kuwa mwanamke huyo pia amekiri kuwa alimlisha mtoto huyo damu ya hedhi kutokana na hasira iliyosababishwa na jinsi mume wake anavyomdekeza mtoto huyo
” Hukumu hii itawashawishi wanawake wengine kufanya sawa na aliyoyafanya huyu wakijua kuwa hukumu yake sio nzito ,” alisema Bi Susan mayanja katibu wa kijiji cha Kitega.
Aliwashauri wanawake kuwalea watoto wa kambo kwa upendo kwasababu hawajui hali yao ya baadae.
No comments:
Post a Comment