We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Tuesday, September 3, 2019

Wanafunzi wanne, mwalimu na mlinzi kortini kwa tuhuma za mauaji ya mwanafunzi mwenzao

Wanafunzi wanne, mwalimu pamoja na mlinzi wa Shule ya Sekondari Katoro Islamic, wamefikishwa Mahakama ya Wilaya ya Bukoba mkoani Kagera wakikabiliwa na tuhuma za mauaji ya mwanafunzi wa kidato cha nne katika shule hiyo, Mood Muswadiku.
Wanaokabiliwa na kesi hiyo ya mauaji namba 18/2019 ni wanafunzi Husama Ramadhan (17), Sharifu Huled (19), Abdallah Juma (19) na Hussein Mussa (20), mwalimu Majaliwa Abud (35) na Badru Issa Tibagililwa (27) ambaye ni mlinzi. Kesi hiyo iliyotajwa jana mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Manispaa ya Bukoba, Frola Kaijage, imeahirishwa hadi Septemba 16, na watuhumiwa hawakutakiwa kujibu kutokana na mahakama hiyo kutokuwa na mamlaka ya kuisikiliza.
Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Chema Maswi, alidai mahakamani hapo kuwa mauaji hayo yalitokea Aprili 14, mwaka huu katika Shule ya Sekondari Katoro Islamic, Halmashauri ya Bukoba mkoani Kagera. Watuhumiwa wamerudishwa rumande hadi hadi kesi hiyo itakapokuja kutajwa tena kwa siku itakayopangwa na mahakama.
Chanzo Mtanzania digital

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list