We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Friday, September 27, 2019

Vituo vya televisheni mtandaoni vyapewa adhabu na TCRA


Kamati ya maudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imeifungia televisheni ya mtandaoni ya Kwanza kwa muda wa miezi 6 baada ya kukutwa na hatia ya kutoa taarifa inayohusu Dk Gwajima kupata ajali bila kutaja jina la kwanza jambo lililoelezwa kufanywa kwa makusudi kuikuza habari

Pia TCRA imezitoza faini ya Tsh. Milioni na kuwapa onyo televisheni mtandao za Millard Ayo na Watetezi TV kwa makosa ya kutochapisha sera na mwongozo wa watumiaji katika chaneli yake za YouTube.

Akisoma uamuzi wa kamati Makamu mwenyekiti  Joseph Mapunda amesema Kwanza Tv wamekutwa na kosa la kukiuka misingi ya uandishi wa habari na kanuni za utangazaji kwa kuchapisha habari iliyolenga kupotosha.

Amesema kupitia ukurasa wake facebook Kwanza tv iliweka video iliyobebwa na kichwa cha habari Dk Gwajima apata ajali.

Mapunda amesema kwa makusudi habari hiyo haikutaja jina la kwanza la Dk Gwajima hivyo kuzua taharuki hasa ikizingatiwa kuna mtu mwingine maarufu anayetumia jina hilo.

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list