We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Sunday, September 15, 2019

Tutawachukulia hatua wanaovunja Sheria - IGP Sirro


Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro amesema kuwa wataendelea kuwachukulia hatua kali za kisheria watu wanaojihusisha na vitendo vya kihalifu ikiwemo kujihusisha na uvuvi haramu kwenye bwawa la nyumba ya Mungu.

IGP Sirro amesema hayo wakati alipofanya ziara ya ukaguzi katika wilaya za Mwanga na Hai mkoani Kilimanjaro, ambapo amewataka wananchi kutii sheria zilizopo ili kujiepusha kuingia mikononi mwa vyombo vya dola.

Aidha, IGP Sirro amewataka maofisa na askari kuzingatia weledi wanapotekeleza majukumu yao na kuhakikisha wanatoa huduma bora kwa wateja.

Akizungumza wakati wa wa ziara hiyo ya Mkuu wa Jeshi la Polisi, Mkuu wa Wilaya ya Hai Mhe. Lengai Ole Sabaya amesema kuwa ni heshima kubwa kwa kiongozi wa Jeshi la Polisi kutembelea kwenye wilaya yake huku akiahidi kuwa, wataendelea kushirikiana na Jeshi hilo katika kudhibiti vitendo vya uhalifu na wahalifu katika Wilaya hiyo.

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list