We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Sunday, September 15, 2019

Azam Fc yashindwa kutumia uwanja wa nyumbani, yafungwa na Wazimbabwe

Azam Fc imeanza vibaya mchezo wa kwanza wa kombe la Shirikisho raundi ya kwanza, baada ya kukubali kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Triangle United ya Zimbabwe
Licha ya kutawala mchezo huo kwa muda mwingi, safu ya ushambuliaji ya Azam Fc ilikosa umakini na kupoteza nafasi nyingi za kufunga
Bao pekee la Triangle United lilifungwa na Ralph Kawondera
Triangle United imemaliza rekodi ya Azam ya kutofungwa katika uwanja wa Chamazi
Mabingwa hao wa kombe la FA watalazimika kupata ushindi kwenye mchezo wa marudiano ugenini ili waweze kusonga mbele
Yanga na Azam Fc ndio timu pekee zilizobaki kwenye michuano ya CAF kutoka Tanzania baada ya Simba na KMC kutolewa katika hatua ya awali
Jana Yanga ililazimishwa sare ya bao 1-1 na Zesco United kwenye michuano ya ligi ya mabingwa
Nayo inahitaji matokeo ya ushindi au sare ya kuanzia mabao mawili ugenini ili iweze kusonga mbele hatua ya makundi

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list