Kikosi cha Simba kimeondoka Bukoba kuelekea jijini Mwanza ambako kitaweka kambi ya siku moja kabla ya kuifuata Biashara United mkoani Mara kwa ajili ya mchezo wa ligi kuu ya Vodacom Jumapili
Taarifa iliyotolewa na uongozi wa Simba mapema leo, imesema Simba itaelekea Musoma kesho
"Kikosi leo asubuhi kinaondoka Bukoba kwenda jijini Mwanza ambako kitakuwepo kwa siku moja na Jumamosi kitaenda Musoma kufanya mazoezi ya mwisho kabla ya mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Biashara United ambao utapigwa Jumapili kwenye Uwanja wa Karume"
Mabingwa hao watetezi, wameondoka Bukoba huku wakiacha simanzi kwa wenyeji wao Kagera Sugar baada ya kuwafumua mabao 3-0 jana
Mchezo dhidi ya Biashara United utapigwa kwenye uwanja wa Karume, Musoma
No comments:
Post a Comment