Washtakiwa watano wanaokabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi akiwemo wakili, Dk Ringo Tenga wamemwandikia barua Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Tanzania (DPP) kuomba kukiri makosa yao.
Wakili wa washtakiwa hao, Byrson Shayoameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Ijumaa Septemba 27, 2019 wakati kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kutajwa.
Dk Ringo ambaye ni Mkurugenzi na mwanasheria wa kampuni ya Mawasiliano ya Six Telecoms Limited na wenzake wanakabiliwa na mashtaka sita, likiwemo la kutakatisha fedha na kuisababishia Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA) hasara ya Dola za Marekani 3,748,751.22.
Mbali na Dk Tenga, washtakiwa wengine ni Hafidhi Shamte au Rashidi Shamte ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hiyo, Mfanyabiashara na Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Peter Noni, Mkuu wa fedha wa kampuni hiyo Noel Chacha na Kampuni ya Six Telecoms.
No comments:
Post a Comment