Kamanda wa Polisi Mkoani Kigoma Martin Ottieno, amethibitisha kutokea kwa tukio la kufa kwa Ng'ombe takribani 22, baada ya kupigwa na radi katika Kijiji cha Kaziramihunda Wilayani Kakonko Mkoani humo.
Kamanda Ottieno amesema kuwa tukio hilo lilitokea juzi Septemba 1, 2019, majira ya jioni wakati Ng'ombe hao wakitoka kunywesha maji kijiji jirani, ambapo ghafla ilinyesha mvua kubwa iliyopelekea tukio hilo.
''Ni kweli tukio hilo limetokea na kulikuwa na makundi mawili ya Ng'ombe, kundi la kwanza lilikuwa na Ng'ombe 16 na mmiliki wake anaitwa Abdul kasungu na kundi la pili kulikuwa na Ng'ombe 6 wanaomilikiwa na Filbert Chibedese na walikuwa wanatoka marishoni, ghafla mvua ikaanza kunyesha, radi ikatokea na kuua mifugo yote 22'' amesema Kamanda Ottieno.
Aidha imeelezwa kuwa katika tukio hilo, hakuna madhara yoyote yaliyotokea kwa binadamu, hususani waliokuwa wanachunga hiyo mifugo.
No comments:
Post a Comment