Uongozi wa Yanga umetimiza ahadi ya kuwapatia wachezaji kiasi cha shilingi milioni 50 baada ya kufanikiwa kuwaondosha Township Rollers ya nchini Botswana katika mchezo wa klabu bingwa barani Afrika.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano, Saad Kimji amesema fedha hizo atakabidhiwa Meneja Hafidh Saleh kwa ajili ya kuziwasilisha kwa wahusika.
Kimji amesema lengo la uongozi ni kuona wachezaji wanatimiziwa mahitaji yao ili na wao waweze kuyafanya majukumu yao kwa ufasaha.
Kabla ya kuwavaa Township Rollers kwenye mechi ya pili, uongozi wa Yanga ulitoa ahadi ya kuwapa wachezaji na benchi la ufundi kiasi hicho cha fedha hizo endapo wangefanikiwa kusonga mbele kwenye mashindano hayo,jambo ambalo walilitimiza
We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.
Subscribe to our RSS feed to stay updated on our progress.
No comments:
Post a Comment