MTOTO wa mfalme wa Saudi Arabia amesema anahusika katika mauaji ya mwandishi wa habari Jamal Khashoggi mwaka jana kwa vile jambo hilo lilifanyika akiwa analifahamu.
Mohammed bin Salman ambaye ndiye mtawala wa nchi hiyo ya kifalme, hajazungumzia hadharani kuhusu mauaji hayo yaliyofanyika katika ubalozi wa Saudia mjini Istanbul, Uturuki. Shirika la ujasusi la Marekani (CIA) na baadhi ya serikali za mataifa ya Magharibi yamesema aliamuru mauaj hayo, lakini watawala wa nchi hiyo wamesema hakuhusika.
Mauaji hayo yalilaaniwa vikali duniani na kuichafua taswira ya nchi hiyo, hali ambayo imemfanya mtawala huyo asiweze kuzitembelea Marekani na nchi nyingine za Ulaya.
“Mauaji hayo yalifanyika mbele yangu, Ninahusika kikamilifu kwani niliyashuhudia,” alisema Salman ambapo ni mwaka mmoja umepita tangu kufanyika mauaji hayo.
Khashoggi, mwandishi wa habari wa gazeti la a Washington Post, alionekana mara ya mwisho katika ubalozi wa Saudia mjini Istanbul, tarehe 2 Oktoba mwaka jana ambako alikwenda kukamilisha mlolongo wa hati za ndoa yake. Mwili wake unasemekana ulikatwakatwa vipande na kuondolewa katika jengo hilo la ubalozi ambapo mabaki yake hayajapatikana hadi leo.
No comments:
Post a Comment