Mwili wa Rais wa zamani wa Zimbabwe, Robert Mugabe leo Septemba 27 unatarajiwa kuchukuliwa kutoka katika jumba lake kuu la mjini Harare na kupelekwa katika kijiji chake, kilichopo umbali wa kilomita 90 magharibi mwa mji mkuu kwa ajili ya mazishi.
Hatua hiyo imekuja kufuatia mvutano ulizuka baada ya Serikali kupendekeza mazishi katika uwanja wa Kitaifa wa Mashujaa katika mji mkuu wa Harare, wakati familia ilisisitiza kuwa mazishi yake yatakuwa binafsi katika nyumba ya Mugabe na ilitaka mazishi hayo yawe ya faragha na yahudhuliwe na wanafamilia pekee.
Inaelezwa kuwa watu wengi katika familia ya Mugabe wana uchungu juu ya kuondolewa kwake madarakani karibu miaka miwili iliyopita na na nafasi yake kuchukuliwa na Emmerson Mnangagwa.
Siku ya jana Serikali ya Zimbabwe ilitangaza kwamba Rais huyo wa zamani atazikwa nyumbani kwake Zvimba kama ilivyoombwa na familia yake na hatapelekwa tena kwenye eneo maalum ambalo lilikuwa limejengwa kwa ajili yake.
"Serikali inashirikiana na familia ya Mugabe katika msimamo wao mpya na msaada wote muhimu utatolewa ili kumpa Rais mazishi yanayostahili kuongozwa na familia'', imeeleza taarifa ya Msemaji wa Serikali Nick Mangwana.
Familia haikutoa sababu ya mabadiliko ya mipango, ambapo hapo awali ilikubali mwili wake kuzikwa katika makaburi ya mashujaa wa taifa hilo na sehemu hiyo maalumu ilikuwa imeanza
kuandaliwa.
kuandaliwa.
Rais Robert Mugabe alifariki dunia Septemba 6 akiwa na umri wa miaka 95 nchini Singapore alikokuwa akipatiwa matibabu.
No comments:
Post a Comment