UPANDE wa mashtaka umeieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa upelelezi wa kesi inayomkabili Blogger, Shamim Mwasha (41) na mumewe, Abdul Nsembo (45) bado haujakamilika hivyo umeiomba mahakama ipange tarehe nyingine ya kusikilizwa.
Hayo yameelezwa na Wakili wa Serikali, Wankyo Simon, mbele ya Hakimu Mkazi, Kelvin Mhina, wakati kesi hiyo ilipoitishwa kwa ajili ya kutajwa. Wankyo amedai kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika hivyo anaomba ahirisho la kesi hiyo.
Hata hivyo, upande wa utetezi ukiongozwa na wakili Charles Kisoka umeomba upande wa mashtaka kuharakisha upelelezi huo. Katika majibu yake Wankyo amesema watajitahidi kuharakisha upelelezi huo.
Hakimu Mhina ameutaka upande wa mashtaka uharakishe upelelezi huo ambapo ameiahirisha kesi hiyo hadi Oktoba 11 mwaka huu na washtakiwa wamerudishwa rumande.
Washtakiwa wanatuhumiwa kukutwa na kusafirisha dawa za kulevya, Mei 1, 2019.
No comments:
Post a Comment