We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Thursday, September 26, 2019

Mkuu wa Mkoa Apiga Marufuku Kuishangilia Simba

Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Brigedia Jenerali Michael Gaguti.
MKUU wa Mkoa wa Kagera, Brigedia Jenerali Michael Gaguti, amepiga marufuku wananchi wa mkoa wake kuishangilia Simba, pindi itaposhuka uwanjani leo kuvaana na Kagera Sugar.

Gaguti amefikia hatua hiyo akiwa na lengo la kuanzisha kampeni ya kuwahamasisha wananchi kuipenda timu yao na kuisapoti pindi itakapokuwa ikicheza na timu kubwa katika michezo yote ya ligi kuu msimu huu.

Kagera itakuwa katika Uwanja wa Kaitaba, kuvaana na Simba, ikiwa ni Mara ya kwanza timu hizo zinakutana msimu huu.


Akizungumzia hatua hiyo Gaguti alisema: “Umefikia wakati wa watu wa Mkoa wangu wa Kagera kuungana na kuisapoti timu yetu inapocheza na timu yoyote katika Uwanja wa Kaitaba na hatua hiyo inaanza kesho (leo) pindi Kagera Sugar itakapocheza na Simba, mkiwa huko pembeni shangilieni hizo timu zenu, ila hapa wote tunaishangilia Kagera Sugar.”

Kwa upande wa Meneja wa Simba, Patrick Rweyemamu amesisitiza wamejipanga kushinda mchezo huo na wala hawana mchecheto wowote.

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list