Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula amezitaka mamla za Miji zote nchini kuhakikisha zinatenga maeneo maalumu kwa ajili ya wafanyabiashara wadogowadogo ili kuepusha migogoro ya matumizi ya ardhi katika Miji yao.
Dkt. Mabula ameyasema hayo Wilayani Igunga Mkoani Tabora wakati akijibu maswali ya wananchi ambao waliwasilisha kero zao kwake, kwani kumekuwepo na migogoro baina ya wafanyabiashara wadogowadogo na baadhi ya mamla za Miji hii inatokana na Mamlaka hizo kutokutenga maeneo maalumu kwa ajili ya wafanyabiashara hao.
“ Lazima kila mamlaka ya Mji iweke utaratibu wa kuwatengea maeneo wafanyabiashara ili waweze kufanaya biashara zao katika maeneo maluumu na sio kuwafukuzafukuza, sasa mnawafukuza ili wakafanye biashara wapi wakati hamja watengea maeneo ya kufanya biashara zao” Amesema Dkt. Mabula.
Dkt. Mabula amesisitiza kuwa nilazima mamlaka za miji ziweke mipango maalumu ya miji yao kwa kutenga maeneo ya biashara ,maeneo makazi maeneo ya kufugia maeneo ya michezo maeneo ya umma na maeneo ya taasisi za dini ili kuepusha migogoro ya matumizi ya ardhi na kuepusha kero kwa wananchi kwa kuwahamisha hamisha mara kwa mara.
Akiwa Wilayani Igunga Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula alifanya mkutanao wa hadhara katika viwanja vya kumbukumbu ya Sokoine na kusikiliza kero za migogoro ya ardhi ya wakazi wa Wilaya hiyo, ambapo wananchi walijitokeza na kumfikishia malalamiko yao ya muda mrefu yanayohusu matumizi ya ardhi .
Miongoni mwa wananchi hao ni Bw. Joseph Kamanga ambae ni fundi seremala anaejihusisha na uuzaji wa vitanda alimuwasilishia malalamiko yake kwa niaba ya vijana wanaojihusisha na uchongaji wa vitanda Naibu Waziri Mabula dhidi ya mamlaka ya Mji wa Igunga kushindwa kuwapatia maeneo maalumu kwa ajili ya biashara zao hali inayopelekea kufukuzwa kila wanapokuwa kwenye shughuri zao.
Ziara hiyo ya Dkt. Mabula ni muendelezo wa ziara zake za kila Wilaya kutatua migogoro ya ardhi na kuhamasisha ukusanyaji wa maduhuri ya Serikali kupitia kodi ya pango la ardhi pamoja na kukagua masijara za ardhi.
No comments:
Post a Comment