Waziri wa Habari sanaa utamaduni na michezo Dokta Harrison Mwakyembe ametoa agizo la kuwasaka kubaini na kuwakamata washereheshaji wa harusi maarufu kama mc mkoani Kagera ambao hawana vitambulisho vya kazi hiyo na kuwa atakayebainika atachukuliwa sheria kali ikiwemo harusi hiyo kusimama wakati huo.
Waziri Mwakyembe ametoa kauli hiyo August 30 Mwaka huu wakati akiwa mkoani Kagera katika mkutano na wadau wa sekta ya habari utamaduni sanaa na michezo uliofanyika katika ukumbi wa mkoa uliopo Bukoba manispaa mkoani hapa.
Waziri Mwakyembe amesema kuwa tayari serikali imeishaweka utaratibu wa kila mfanya biashara kuwa na kitambulisho na kudai kuwa utaratibu huo unajulikana nchi nzima.
Ametaja kuwa kitendo cha baadhi ya washereheshaji kunyonya jasho la ambao tayari wamelipia vitambulisho vya kuwatambua katika kazi hiyo ni kosa kisheria.
Waziri huyo Amesema ni jambo la kusikitisha na kutoa agizo la Wakaguzi kufanya msako mkali ili kubaini washereheshaji ambao hawajasajiliwa na kuwa wakibainika watachukuliwa sheria kali ikiwemo harusi hiyo kusimamishwa wakati huo.
Amesema sambamba na kuwachukulia sheria kali watatozwa Faini itakayo ingizwa katika mfuko wa wasanii ili kuinua tasnia ya utamaduni na sanaa.
No comments:
Post a Comment