Serikali ya Msumbiji inatarajia kutumia Dola za Marekani $325,000 sawa na Tsh. milioni 750 kwa ajili ya maandalizi ya ziara ya Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis wiki ijayo.
Redio ya serikali ndiyo iliyotangaza kiwango hicho cha fedha na kueleza kuwa kila mmoja ameonekana kufurahia ujio wa kiongozi huyo.
“Kuna bajeti ya msingi, lakini inarekebishwa, ukizingatia kuwa wakati mambo kama haya yanafanywa, kuna hali fulani ambazo zinahitaji kushughulikiwa,” Waziri wa Mambo ya Nje, Jose Pacheco aliiambia Redio Msumbiji, akithibitisha kiwango hicho.
Papa Francis anatarajia kuitembelea Msumbiji, ambapo atakwenda pia Madagascar na Mauritius kati ya Septemba 4-10.
Msumbiji, ambayo ilikuwa koloni la Ureno ina takribani Wakatoliki milioni 4. Ziara hiyo ya Papa inatokana na mwaliko aliopewa Septemba 2018 na Rais Filipe Nyusi.
No comments:
Post a Comment