We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Monday, September 2, 2019

JPM awataka watendaji Kata, wawasimamie Mawaziri

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewataka Watendaji Kata nchi nzima, kusimamia vema miradi ya Serikali ambayo inatekelezwa kwenye maeneo yao.

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo Ikulu, jijini Dar es salaam, wakati akizungumza na watendaji hao wa kata, ambapo amewataka licha ya kusimamia miradi ya Serikali, pia kusimamia nidhamu ya watumishi wote wa umma wakiwemo Mawaziri Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya, wanaoishi kwenye Kata zao.
"Nyinyi ndiyo wasimamizi wa Watumishi wa Umma kwenye Kata zenu, Mtumishi wa Umma aliyeko kwenye Kata yako, wewe ndiye msimamizi wake, kama kwenye Kata yako yuko RC, Waziri au DC usiogope kumwandikia mapendekezo kama anaenda kinyume na maadili ya kazi zake na ukimuona mkubwa sana nitumie nakala na mimi". amesema Rais Magufuli.
Aidha Rais Magufuli amesema kuwa "mradi wowote utakaosimamiwa Kitaifa wewe unahusika, mtu akikwambia unasimamiwa Kitaifa mwambie Kitaifa ni pamoja na wewe, ukiona fedha zinachezewa piga filimbi wewe ni bosi, sababu ya kuwaita hapa ni kuwapa hayo meno nyinyi ni mabosi, sasa atokee mwingine aseme nyinyi sio mabosi mwambieni aje kuniambia mimi hivyo".
Rais Magufuli amesema kikao hicho ni mwendelezo wa vikao mbalimbali anavyofanya na Watumishi wa Umma, Ikulu, ambapo lengo lake kusimamia miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali.

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list