Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amezungumzia kuhusu kuhusu sheria mpya ya mavazi ya benchi la ufundi kwa klabu za Ligi Kuu Tanzania bara, Ligi Daraja la Kwanza na Ligi Daraja la Pili.
Katika waraka wa marekebisho ya Ligi Kuu 2019/20 uliotolewa Agosti 21, kanuni ya 14 kipengele cha 2m kinaeleza kuwa kocha mkuu na viongozi wa benchi la ufundi wanawajibika kuvaa sare maalum kwa timu yao kwa benchi la ufundi.
Kipengele hicho kinaendelea kueleza kuwa endapo kocha mkuu atahitaji kuvaa mavazi mavazi tofauti, anawajibika kuwa katika mavazi ya heshima na nadhifu, ikisisitiza kuwa ukiukwaji wowote utavutia adhabu kwa mhusika.
Kanuni hiyo imeonekana kumlenga zaidi Zahera ambaye amekuwa akivaa mavazi tofauti tofauti ikiwemo pensi anaposimama uwanjani timu yake ikicheza. Mwenyewe amejibu akisema, "Duniani kote katika soka hakuna sheria ya mavazi kuwa kocha anatakiwa avaaje, vile mimi navaa nakua najihisi vizuri".
"Kuhusu mavazi, kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp ndiye kocha anayevaa hovyo, ila kama wamebadilisha sheria kwa ajili ya Zahera basi mchezo ujao nitavaa suti", ameongeza.
No comments:
Post a Comment