Kuanzia mwezi wa kumi, klabu ya Simba huenda ikaanza kutumia uwanja wake wa Bunju ambao uko kwenye hatua za mwisho kukamilika
Simba imetengeneza viwanja viwili Bunju, kimoja kikiwa cha nyasi asili na kingine cha nyasi bandia
Kiwanja chenye nyasi asili, kiko kwenye hatua za mwisho kabisa kukamilika
Uongozi umesema mpaka Oktoba huenda Simba ikaanza kujifua katika uwanja huo
Kukamilika kwa viwanja hivyo kutaifanya Simba iondikane na gharama za kukodi viwanja vya mazoezi
Aidha baada ya kukamilika kwa awamu ya kwanza ya ujenzi huo, awamu ya pili itawahusishwa wadau wa Simba ambao watashirikishwa kuchangia ili kuhakikisha uwanja huo unakamilika haraka na kuwa uwanja rasmi wa Simba kwa ajili ya michezo ya ligi na mashindano mengine kadiri itakavyoonekana inafaa
No comments:
Post a Comment