Mtendaji Mkuu wa Simba Senzo Mazingiza leo atakuwepo uwanja wa Kaitaba kushuhudia mchezo wa ligi kuu ya Vodacom kati ya Kagera Sugar dhidi ya Simba
Mazingiza ameondoka mapema leo kuelekea Kagera kwa ajili ya mchezo huo ambao utapigwa saa kumi jioni
Kikosi cha Simba kiko mkoani Kagera tangu jana ambapo jioni kilifanya mazoezi ya mwisho kwenye uwanja wa Kaitaba
Mchezo huo unasubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soka nchini

No comments:
Post a Comment