We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Thursday, August 29, 2019

Waziri kuwachukulia hatua wanaotoa mimba hivi

Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Dkt Faustine Ndugulile, amesema  Serikali itahakikisha inakomesha uuzaji holela wa dawa mbalimbali,  hususani zile zinazotengenezwa kwa ajili ya matumizi mazuri na kugeuzwa kuwa ni za kutolea mimba.

Waziri Ndugulile ameyabainisha hayo leo Agosti 29,  baada ya Kamati ya Bajeti ya Bunge la Baraza la wawakilishi Zanzibar,  kutembelea Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba Nchini Yaani (TMDA).
"Hizi dawa zinazoitwa Misoprostol ni dawa ambazo zinatumika katika uzazi kuongeza uchungu na kupunguza uvujaji wa damu,  lakini dawa hizi hizi katika matumizi yake mabaya zinaonekana zinaweza kusaidia kutoa ujauzito na hilo sasa hivi limeonekana kuwa ndiyo tumizi kuu kuliko lile tumizi la kwanza, lengo na kusudio la dawa lilikuwa ni zuri lakini sasa ni tofauti kwahiyo wajibu wetu kama Serikali ni kusimamia vizuri ". Amesema Dkt Ndugulile.
Aidha Serikali imesema itawachukulia hatua kali zaidi,  wauzaji wote  wanaouza dawa bila kutumia cheti cha daktari na kwamba serikali itaanzisha msako mkali.

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list