We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Friday, August 16, 2019

Polisi Yavamia Mkutano wa Zitto, Yamkamata Msemaji ACT

Jeshi la Polisi limevamia makao makuu ya chama cha ACT Wazalendo yaliyopo Kijitonyama jijini Dar es Salaam na kuzuia mkutano wa Kiongozi Mkuu wa chama hicho, Zitto Kabwe, aliokuwa aufanye leo Ijumaa, Agosti 16, 2019 na wanahabari ofisini hapo.
Polisi pia, wamemkamata Katibu wa Uenezi wa chama hicho, Ado Shaibu,  na kuelekea naye kituo cha Polisi Oyster Bay, jijini Dar es Salaam kwa mahojiano.
Naibu Katibu wa Uenezi ACT Wazalendo, Seif H. Suleiman,  amethibitisha tukio hilo na kusema magari mawili ya askari polisi wakiwa na silaha walifika ofisini hapo na kuzuia mkutano huo ambapo dakika takribani 15, waliondoka na Ado Shaibu.
Leo, Zitto Kabwe alitarajia kuongea na waandishi wa habari kuhusu Mkutano Mkuu wa 39 wa Wakuu wa Nchi za Jumuia ya Maendeleo ya Nchi za Kusdini mwa Afrika (SADC).
Mkutano huo umeahirishwa mpaka taarifa nyingine zitakapotolewa.

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list