We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Friday, August 16, 2019

Tuko tayari kuikabili Azam Fc , Mwarami awataja wachezaji watakao ukosa mchezo wa Azam fc

Kocha wa makipa wa kikosi cha mabingwa wa soka Tanzania Bara Simba, Mwarami Mohammed amesema timu iko tayari kwa mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Azam Fc ambao utapigwa kesho Jumamosi kwenye uwanja wa Taifa
Akizungumza kuelekea mchezo huo kwa niaba ya kocha Patrick Aussems, Mwarami amesema SImba ina matumaini makubwa ya kufanya vizuri kwenye mchezo huo kutokana na maandalizi makini waliyofanya
"Tuliweka kambi yenye mafanikio Afrika Kusini kwani kule tulicheza michezo kadhaa ya kirafiki ambayo tulifanya vizuri," amesema
"Tukarejea nchini na kufanya vizuri kwenye mchezo wa kilele cha Sportpesa Simba Week kisha kuelekea Msumbiji ambako hatukupata matokeo mabaya"
"Kimsingi tuko tayari kwa mchezo wa kesho na tunawaomba mashabiki wetu waje kwa wingi kutuunga mkono"
Kuhusu hali za wachezaji, Mwarami amesema ni wachezaji watatu tu ambao watakosa mchezo huo kutokana na majeruhi
"Wachezaji wako vizuri isipokuwa Aishi Manula, Ibrahim Ajib na Wilker ambao ni majeruhi"
Mchezo huo unatarajiwa kuanza saa moja jioni

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list